| Mama Salma Kikwete akitoa zawadi kwa wageni waliofika kufuturu Ikulu ndogo la Lindi leo |
| JK akitoa neno la shukrani kwa wageni wake baada ya futari |
JK akiongea na wakwe zake baada ya kufuturu na wananchi wa Lindi
| Mwakilishi wa Globu ya Jamii Mtwara na Lindi, Mdau Abdulaziz Video baada ya kusalimiana na JK |
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwasili uwanja wa ndege wa Lindi.
Nyuma yake ni Mkuu wa Mkoa huo Mh. Meck Sadiki.
Kufuatia tatizo sugu la maji lilodumu kwa muda mrefu katika halmashauri ya manispaa ya Lindi,Rais Kikwete amewaagiza madiwani wa halmashuri hiyo kukaa kwa pamoja na mamlaka ya maji safi na maji taka Lindi(LUWASA) ili kuzungumza na kufikia muafaka wa kumaliza tatizo hilo la maji.
Rais Kikwete ametoa agizo hilo katika futari ya pamoja na wakazi wa mkoa wa lindi iliyofanyika nyumbani kwake, na kuitaka halmashauri ya Manispaa Lindi kuikopesha fedha LUWASA shilingi milioni 12 kila mwezi hadi Mwezi Disemba mwaka huu kwa ajili ya kusaidia kupunguza tatizo la maji,na baadaye fedha hizo zitarudishwa na wizara ya Maji. Picha na habari na Abdulaziz Video wa Globu ya Jamii, Lindi


That's JK bwana! Very good! Kila m2 anapendeza t-shirt na jeans.
ReplyDelete