Abiria wa kwanza kusafiri na Precision Air kutoka Comoro walionekana kufurahia huduma hiyo ya ndege.  Jumla ya abiria walikuwa 110, ndege iliyofanya safari hiyo ni aina ya Boeing 737-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 116.
 Afisa Mawasiliano wa Precision Air, Bw. Amani Nkurlu akiwa na wana anga wa shirika la ndege hilo walioshiriki kufanikisha safari ya kwanza ya kwenda na kurudi Hahaya, Comoro,  kutokea Dar es Salaam jumatano iliyopita.

 Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akisindikizwa kwenda kupanda ndege na wenyeji wake baada ya uzinduzi mfupi uliofanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Prince Ibrahim, mjini Hahaya, Comoro. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi wa serikali ya Komoro Bw. Abdulahi Mwinyi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi mfupi iliyofanyika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Prince Ibrahim aliishukuru shirika la ndege la Precision Air kwa hatua ya kuanza safari nchini mwao. “Hakika hii ni fursa nzuri ya kuendeleza ushirikiano endelevu uliopo baina ya nchi zetu mbili. Bila shaka wakomoro watapata usafiri wa anga wa uhakika hasa hasa katika kuendeleza sekta ya biashara,” alisema.
 Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse (kulia) akikaribishwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi nchini Komoro Bw. Abdulahi Mwinyi mara baada ya kuwasili na safari ya kwanza ya shirka ya ndege hiyo kutokea uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko akiteta na Mwenyekiti wa Galaxy General Sales Agents, Bw. Nassor Ali. Kampuni ya Galaxy ni wakala rasmi wa Precision Air nchini Comoro.
Ndege aina ya Boeing 737-300 ilivyotua kwa mara ya kwanza uwanja wa ndege wa kimataifa wa Prince Ibrahim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. NAAANDIKA HAYA KWA UCHUNGU MKUBWA KWA NCHI YANGU TANZAGIZA. KWANZA NAWAPA BIG UP SANA PRECISION AIR KWA KAZI NZURI. HIVI TANZAGIZA KUNA SHIRIKA LA NDEGE LA SERIKALI ??? NI AIBU ILIYOJE NCHI KUKOSA MAMBO MUHIMU. WENZAKO KENYA SASA HIVI NDEGE ZAO ZINAPEPEA DUNIA NZIMA. TANZAGIZA BADO TUPO MIAKA YA 47 KILA MTU UKIMUULIZA MJUAJI. JARIBU TU KUTAFUTA YOUTUBE AU GOOGLE AIR TANZAGIZA KAMA UTAPATA LA MPWASHO. JAMANI WAKENYA WANATUACHA. TANZAGIZA HATA REDIO ONLINE PIA SHIDA ZAIDI YA BONGO REDIO NA REDIO TUMAINI KWISHA. TUNAPATA AIBU JAMANI, UUUUWIIIIIII NCHI YANGU TANZAGIZA. MWENYEKITI MAGGID MJENGWA HUWAGA ANATUKUMBUSHA ULE MSEMO WA MWANAFALSAFA WA KIYUNANI KWAMBA 'KILA KUKICHA KUTAZUKA KIOJA KIPYA AFRIKA' ILA MIMI NAPENDA NIUBINUE KIDOGO HUU MSEMO, TUSEME TU YA KWAMBA 'KILA KUKICHA KUTAZUKA KIOJA KIPYA HAPA TANZAGIZA'

    ReplyDelete
  2. PrecisionAir ni kampuni ya Kitanzania hivyo hatuna haja ya kupiga kelele bali kuzidi kuwapa moyo PrecisonAir kwa kuchukua jukumu la kuibeba bendera ya Tanzania katika sekta ya usafiri wa anga ndani na nje ya Tanzania.

    Kwa mara nyingine naishukuru PrecisionAir kwa kuiweka Tanzania katika ramani za usafiri wa anga duniani. Makampuni mengine ya kitanzania ktk sekta zingine pia yaamue kuindeleza Tanzania hata bila ya kuwa ni mashirika ya umma kama Air Tanzania au National Milling Corp ambayo sasa AZAM Bakhresa pia inafanya biashara nadani na nje ya mipaka ya Tanzania.

    Tusijione wanyonge kwani Watanzania tunaweza kuwa na makampuni makubwa ambayo siyo mashirika ya umma.

    Mdau
    Kifua-Mbele Mtanzania.

    ReplyDelete
  3. Makampuni tunayo na tutaendelea kuwa nayo kama mtaturuhusu kuendelea na ufisadi serikalini. Nasema hivi kwa sababu kuendelea hadi kuwa na kampuni kama ya Bkhressa Tanzania kunahitaji mtaji mkubwa sana ambao inawezekana kuupata kwa njia halali kama watu wataamua kuingia partnership. Lakini kwa hulka za watz partnership ni ngumu. Kwa hiyo njia pekee ya kujipatia mtaji ni ufisadi na rushwa tu.

    Ninachowaommba tu wale mtakaofanikiwa kukwapua mikwanja ya nchi, makampuni yenu yapeni majina angalau yanayoitangaza nchi. Kwa mfano kwa kuwa Air Tanzania imeshakuwa marehemu, basi Prcission ingeitwa Precission-Tanzania ingekuwa inajitangaza yenyewe na nchi pia.

    ReplyDelete
  4. Nilidhani PrecisionAir inamilikiwa na wabondeni(South Afrika).Naomba mnisaidie.

    ReplyDelete
  5. NYINYI HAPO JUU WADAU WAWILI HAMUNA HABARI KUWA KENYA INA HOLD 49% YA HISA ZA PRECISION AIR,NA WAO NDIO WANAOPIGA PUSH HII KAMPUNI IENDELEE,SISI WABONGO TUTAENDELEA KUBARIKIWA KIPAJI CHA KUPIGA DOMO,UTENDAJI ZERO.

    ReplyDelete
  6. Kuna tafauti kubwa kati ya Kenya na Tanzania. Kenya kuna abiria wengi sana wanaopitia Kenya, uwanja wao ni mkubwa sana, mmiliki mkuu wa Kenya Airways ni KLM, watalii wengi sana wanatembelea, mahoteli mengi sana yanamilikiwa na wazungu, jeshi la marekani na uingereza wana kambi, kila pahala sasa wanatumia electronic payment na mengi. Hata elimu pia wametuzidi. Mkenya ana bidii angalia riadha sasa kwenye mbio ndefu, hawasubiri serikali iwapeleke. Wakalenjini wote sasa wanafanya mazoezi wawe wanariadha.

    ReplyDelete
  7. bla bla bla bongo kwishinehi no maendeleo mpaka viongozi walioanza tokea uhuru wafariki wote wabakie wa leo.

    ReplyDelete
  8. He. Mbona mizigo imekaa wazi. Kikitokea cha kutokea si itawaangukia abiria. Am just thinking loud!

    Hiyo kampuni inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na Kenya Airways kama hamna taharifa. Tz hakuna chetu hapo!

    ReplyDelete
  9. sasa kama Kenya Airways ina 49% tatizo liko wapi? mbona Kenya Airways inamilikiwa 26% na KLM (ukiacha non-Kenyans shareholders kama financial co. na individuals)? Watu wasiojua biashara mawazo mgando mgando tu na unazi (u-nationalism) tu kila kona! Biashara (esp. airline) haiendeshwi na hisia za huyu simpendi na sifanyi nae bisahara bali hali halisi ya soko na pia washirika strategic! Wewe kwa akili yako unadhani PW ingeweza kufurukuta mbele ya KQ na ET katika ushindani wa soko la EA? Hebu tuambie Air Tanzania ipo wapi (ikumbukwe nao wali-partner na SA Airways) na itakuwa wapi kama haitakuwa na strategic partners! Labda kama serikali yako ina uwezo wa kutoa US$ 500 million na isiweke mijitu toka Machokoroni isiyo na idea ya kuendesha airline! Otherwise haiwezi kuhimili ushindani

    ReplyDelete
  10. NATIONAL CARRIER!

    ReplyDelete
  11. Jamaa wanatoa luggage allowance 46 kg. wow....!

    ReplyDelete
  12. Nachukizwa kweli na watu mnaopenda kusifia vya wengine na kushindwa kuthamini vya kwenu. Lini hii hali mtaachana nayo?

    Kuna mdau hapo juu kasema hiyo kampuni inamilikiwa na wakenya kwa kiasi kikubwa. Sio kweli. Hii ni kampuni ya watanzania karibia wote. Na kama yupo mkenya ni jambo la kawaida kwenye biashara. Hata ndege za Kenya airways (KQ) sio zote zinamilikiwa na wakenya. Kenya ina asilimia 23 tu zingine zinamilikiwa na wazungu. Naona kila kitu mnasifia Kenya tu. Tunayo mengi sana ya kujivunia ambayo hakuna nchi yoyote Africa inayo lakini hamtaki kuakuza mnakuza wakenya. Ovyoooo!

    ReplyDelete
  13. Huyo anayesema mizigo itaangukia watu hajafikiri kabla ya kuandika. Kwani umeona hiyo ndege ipo kwenye mwendo? Ndege imesimama mizigo itaangukiaje watu? Itakapokaribia kuondoka watafungia mizigo.

    ReplyDelete
  14. Nafikiri huyu anayesema hii kampuni ni ya wakenya anatoka Kenya. Simshangai manake wana tabia ya kutaka kila kitu kizuri kiitwe cha Kenya.

    Mlima Kilimanjaro - Kenya
    Serengeti - Kenya
    CD za Bongo flava za watanzania zote zimewekwa anuani za Kenya

    Greed People!!!!

    ReplyDelete
  15. ahahaaaaaa jamani wabongo kwa maoni matamu matamu nawapendaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...