Mkurugenzi wa makampuni ya mbegu Tanzania ,Baldwin Shuma akizungumza na wakulima (Hawapo pichani) wakati wa maonesho ya wakulima yaliyofanyika Kimashuku mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha mbegu ya Northern Seed Co,ltd Arson Shangali akiwaonesha wakulima mashamba mawili ya mahindi yaliyopandwa mbegu tofauti za mahindi.
Wakulima wakiangalia tractor linalotumika kubeba Mahindi mara baada ya kuvunwa shambani siku ya maonesho ya wakulima yaliyofanyika Kimashuku mkoani Kilimanjaro.
Afisa Kilimo na Mifugo kata ya Machame Richard Kessy akitoa ufafanuzi kwa wakulima juu ya mbegu za mahindi zinazo himili uhaba wa mvua kutoka kampuni ya NOSCOL.
Wakulima na wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia maelezo kutoka kwa mmoja wa wazalishaji wa mbegu (hayupo pichani).
Baadhi ya wakulima wakitembelea banda la maonesho ya wakulima kutizama mbegu bora zinazozalishwa na kampuni ya NOSCOL.
Mfanyakazi wa kampuni ya mbegu ya NOSCOL,Reggy Masawe akimuonesha mmoja wa wakulima wa Kimashuku aina bora ya mbegu za mahindi wakati wa maonesho ya wakulima yaliyofanyika Kimashuku mkoaniKilimanjaro.
Wakulima wakiwa katika picha ya pamoja siku ya maonesho.Picha na Dixon Busagaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mahindi yanayotokana na genetic modified seeds sio orgnic, hayana ubora kama mahindi yatokanayo na mbegu za kienyeji, dawa sio kuhimili mvua kidogo kwa sababu kwa mwendo tunaokwenda nao si ajabu katika miaka michache ijayo hata hiyo mvua kidogo hatuiona kwa sababu ya global warming, tukazane na kilimo cha umwagiliaji wa mbegu zetu za kienyeji...tuna maji mengi tu chini ya ardhi.
    haya mambegu ya genetic yatatufanya tupoteze kabisa mbegu zetu za kienyeji...to sad!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...