Mkuu wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu ( mwenye miwani) akiwa na baadhi ya viongozi wakiingia kwenye uwanja ambako zilifanyika sherehe za maadhimisho miaka 10 ya taasisi ya utafiti wa kahawa nchini (TaCRI) uliko katika kituo cj ha utafiti cha Maruku, sherehe hizo zilifanyima jana, kulia kwake ni mwenyekiti wa taifa wa TaCRI vedasto Ngaiza, wa mwisho kushoto ni meneja wa Tacri kanda ya Bukoba Malyatabu ngh’oma na anayefuata ni mkuu wawilaya ya Bukoba samwel Kamote
Baadhi ya maofisa kilimo, wakulima wa zao kahawa na viongozi wa vyama vya msingi walioudhulia sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya TaCRI iliyofanyika kwenye eneo la kituo cha utafiti wa mazao kilichopo Maruku.
mkuu wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu akishangilia baada ya kuzindua jengo la maabara litakalotumiwa na taasisi ya utafiti wa kahawa kuifanyia utafiti miche bora yenye ukinzani na mnyauko fizali.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mohamed Babu akisilikiza kwa makini maelezo toka kwa meneja wa Kanda wa TACRI Malyatabu Ngh'oma ambaye hayuko pichani juu ya namna ya maabara iliyozinduliwa itakavyotumika kuzifanyia utafiti wa kupata miche bora ya kahawa.
.
Mkuu wa mkoa wa Kagera akiendesha trekta litakalotumiwa na TACRI kwa ajili ya kulima mashamba mara baada ya kulizindua, trekta hilo ni la msaada lilitolewa na jumuia ya ulaya. Na Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Kagera
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...