Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. SAFI KITOWEO KIZURI SAFI SANA, MUANZE KUSEMA MBOVU NYIE WADAU WAKATI WENGINE MNAKULA SENENE NA SISI HATULI NA WACHINA WANAKUNA KILA KITU. KITOWEO SAFI KABISA NA MKEMIA MKUU HATA UPINZANI. NTWARA OYE, OYE

    ReplyDelete
  2. girlfriend wangu atakoma kuringa maana kusini ndio kwa wazazi wake lazima hii nirecord nimtanie....chamaki nchanga

    ReplyDelete
  3. Hii ni habari ya kipekee, na inafundisha mambo mengi. Isipokuwa mwandishi/aliyerekodi documentary anatakiwa aongeze umakini kikazi. Hapa anaonekana kama anakejeli zaidi kuliko kutaka kujua na kuifahamisha hadhira.
    Kama hawa watu wamekuwa wakila kitoweo hiki kwa miaka mia kadhaa, basi hawana sababu yoyote ya kuonekana kama ni watu wa ajabu, na waendelee tuu kula. Sisi tuliozaliwa baharini pia kuna watu wanatushangaa sana kwa kula pweza na ngisi. Hivi vyote ni vyakula tuu.

    ReplyDelete
  4. Daah si mchezo Chamaki-Nchanga! , Wasenegal, Hao-hao...... majina kibao ya panya. Safi sana wajasirimali buku 25 kwa tenga zima.

    ReplyDelete
  5. wadau wa ntwara samaani tuelimishane kigodo - hivi chamani anapasuliwa kutoa utumbo au anachomwa hivyo hivyo na utumbo wake?

    ReplyDelete
  6. Panya wanaliwa kila sehemu. Nendeni Dodoma mkawaulize watani zangu wagogo kuhusu utamu wa panya. Wao wanaita "food". Yaani vyakula vingine si vyakula ila panya ndio kaoneka kufaa kuitwa chakula.

    Kule mbeya pia wanakula hao panya na nyungunyungu.

    Ila bora ya Mhehe anayekula mbwa kuliko hawa wanaokula panya.

    Pia bora ya chinga anayekula panya kuliko mchina anaye kula chura.

    Hiki ni chakula tu hakuna kukejeliana.

    ReplyDelete
  7. kwa hii picha ya kutisha sitaenda kusini hata siku moja. ninashukuru nilizaliwa kilimanjaro. kwanini watu wale kitu kama hicho. sitaki hata kusikia any of my relatives wanaoa au kuolewa na watu wa huko. lo ptu mbaka.

    ReplyDelete
  8. Ukifika Lusaka mjini,nchini Zambia "kitoweo" hiki kinauzwa bila shida.

    ReplyDelete
  9. hiki ni chakula cha kawaida kwao amboa kinaweza kuingia kinywani mwao, kwa wale ambao si utamaduni wao hakiwezi kuingia kinywani na hivyo chaweza kuonekana halamu au kisichofaa kuliwa. Wala hakuna sababu ya kujipongeza eti kwa sababu hukuzaliwaw mahali fulani, wakati hata huko tulipozaliwa yapo mambo ambayo hayakubaliki kwa wengine. ndugu zangu tafuneni hao panya kwa uhuru chakula cha jadi yenu na sisi huku tunatafuna senene na tunawasikitikia wasiokula kama ninyi mnavyowashangaa wanaowashangaa!

    ReplyDelete
  10. Mdau wa kilimanjaro unayeshangaa watu wa kusini kula panya. Hiyo ni hali ya kawaida mbona. Kisicho halai kwako ni halali kwa mwenzio. Haya ni mambo ya kawaida kabisa. Mbona Kilimanjaro wachagga wanakula PANYA BUKU au kwa vile yeye ni mkubwa na ana mkia mrefu ndio maana mnamhalalisha?

    Kama wewe si mchaga utakuwa mpare. wapare mnasemwa mnakula ugali kwa picha ya samaki. Si afadhali ya anayekula panya? Hata hivyo nilikuja kugundua kwamba kula ugali kwa picha ya samaki sio kweli ila mlikuwa mnataniwa tu na watani zenu. Nilishaishi kwa wapare sikuwahi kuona wala kusikia jambo hili na wapare walikanusha kwamba wakasema ni utani tu wa wachagga.

    Wakristo wa medhehebu ya wakatoliki, walokole, Aglican na waluter mbona mwala kitimoto wakati kwa muislamu au mkristo msabato hakipandi?

    Viumbe vyote ni chakula tu (kasoro binadamu), ili mradi hakimdhuru mtu.

    ReplyDelete
  11. sisi mbona kwetu tunakula watu.... watu wakifa tunawatoa viungo na kula. Nyama ya mtu ni tamu sana.

    ReplyDelete
  12. Wewe anony wa kuzaliwa kilimanjaro, subiri dada yako akishakatikiwa miuno ya kimakonde kisha uone kama utaweza kumzuia kupika na kula hao wasenegali.

    ReplyDelete
  13. Kusema ukweli hivi vijitu vinatia kinyaa kwa wale tusiokula. Mtu hajanishawishi kuwala. Kwa wanaokula endeleeni kufaidika na kitoweo.

    ReplyDelete
  14. ................... utani utani! nikalishwa senene bwana, wacha tuu wanaladha kama prawns ! naogopa kweli kwenda huko nisijeshawishika kuonja !

    ReplyDelete
  15. hivi hamkupata habari kuwa future foods ni wadudu hebu tafuteni habari. Tatizo watazania vijana hamsomi mambo ya kilimwengu. MNAJIFANYA MNAJUA KUMBE HAMJUI LOLOTE HUYU CHAMAKI NCHANGA NDIO ATAKUWA EXPENSIVE FOOD IN FUTURE. HAWA WANAZALIWA 10 20 KILA WIKI TATU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...