Kwa kutambua umaarufu na umuhimu wa lugha ya Kiswahili duniani, Microsoft wametoa pack ya Kiswahili kwa ajili ya Widows 7 na Microsoft office. Pack hii inapatikana online na zaidi ya yote ni BURE. Akizungumzia toleo hili boss wa Microsoft Afrika Mashariki na Kusini bwana Luis Otieno alisema

“zaidi ya watu million 150 wanaozungumza Kiswahili Afrika sasa wanaweza kuanza kutukia technolojia kwa kutumia lugha waipendayo na kuielewa zaidi. Hii ni mojawapo ya njia za kupanua wigo wa lugha duniani”.

Viongozi na wabia mbalimbali Afrika na duniani kote wameipokea habari hii kwa furaha kubwa. Mkurugenzi wa elimu nchini Kenya mama Lydia Nzomo Windows 7 Ya Kiswahili ni ushindi kwa watoto wa shule za msingi kwani itawasaidia kujua kutumia komputa haraka.

Microsoft wanasema toleo hili litahamasisha serikali za nchi husika kuongeza uwekezaji kwenye mambo ya IT, kupunguza ujinga na kuwavutia watu wengi zaidi kutumia komputa hasa kwenye nchi hizi ambazo utumiaji wa komputa bado ni mdogo.

Kazi ya kutengeneza toleo la Kiswahili lilifanywa na wataaluma wa lugha ya Kiswahili kutoka Afrika mashariki na kati kwa muda wa miaka miwili. Aliyeiongoza kazi hii ni mtafasiri wa lugha ya Kiswahili ndugu Mpasua Msonobari. Mpasua alisema kuna maneno zaidi ya 300,000 yliyotafasiriwa kwa Kiswahili kwenye toleo hilo jipya.

Microsoft wamekuwa wakishirikiana na nchi mbali mbali Afrika na duniani ili kuzitambua na kuzitafasiri lugha mbalimbali.

Habari hii ni nzuri lakini watanzania tujiulize, kama Tanzania ndio mama wa Kiswahili, je, kuna mtanzania aliyeshiriki katika kazi hii?

Pata (Download) Windows 7 toleo la Kiswahili kutoka kwenye blog yako ya teknoloji http://it4dev.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. It was there for download long ago.

    ReplyDelete
  2. sasa hiyo itarudisha maendeleo nyuma kabisa nadhani kiswahili kingekuwa ni kwa ajili ya utalii na mawasilianao ya kawaida ila kikazi nashughuli za kimasomo iwe English kwani itawapa upeo wa kutumia Material nyingi zilizoko kwenye lugha hiyo ya kiingereza.

    ReplyDelete
  3. Haijalishi ikiwa Mtz hajashiriki kufanikisha tafsiri ya hiyo software. Cha muhimu kiswahili kimeanza kutambulika kimataifa zaidi, na pia watu watapata ajira, sidhani km hiyo software itakuwa imekamilika bila mchango wa wataalamu wa kiswahili. Wapo Wakenya, waganda, Wasomali hata Wajerumani pia ni wataalam wa kiswahili, na ninaamini km kutakuwa na makosa kadhaa basi marekebisho yatakuwa yanafanywa kwa consultation na wataalam wa kiswahili wakiwemo Watanzania wenyewe. Kwa hiyo mantik ya Mtz kuwepo ama kutokuwepo sioni km ina mashiko mzee mwenyewe!!

    ReplyDelete
  4. Kitu ambacho watu wanatakiwa kufahanmu ni kwamba hii ni swahili language pack. Ili uweze kuitumia inabidi uwe na "Genuine" Microsoft Operating System au Genuine Microsoft Office. Ambazo inabidi uzinunue ili kuweka language pack. Vinginevyo it doesn't work on it own.

    ReplyDelete
  5. Inategemea kama mwenye hiyo project alimtaka nani afanye hiyo kazi ya tafsiri. Je alitangaza? Kwa hiyo issue siyo kuwa ni kwa nini Watanzania hawakushiriki.... After Tanzania tuko mbali kwa kiswahili na tumefanya kiswahili iwe official language katika umoja wa Afrika na Afrika Mashariki sasa tunaelekea mashariki UN.
    Hakuna matata... Na hata hiyo window7 ya kiswahili ina mapungufu makubwa nionavyo mimi!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...