![]() |
| Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige |
Uamuzi huo ulitangazwa leo bungeni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Ezekiel Maige wakati akifanya majumuisho ya hotuba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2011/12 ambapo Waziri alisema, Mbangwa na wenzake, wamesimamishwa kazi kwa malipo kuanzia leo hadi uchunguzi wa sakata hilo lililowaudhi wabunge na Watanzania wengi utakapokamilika.
Aidha, amesema inaundwa Tume kuchunguza madai ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi ya Ngorongoro, Pius Msekwa ya kugawa viwanja ndani ya hifadhi hiyo kwa wawekezaji ili wajenge hoteli, kinyume cha mamlaka yake.
Maige alisema Tume hiyo itachunguza na kuangalia nini kinafanywa na Bodi na ikigundulika, tuhuma ni za kweli, hatua zitachukuliwa dhidi ya mhusika.



Wamesimamishwa kazi ila bado wanalipwa! sasa si bora waendelee tu na kazi maana inayopata hasara ni serikali hapo. Mi naona serikali inawalinda hawa mafisadi, wanatakiwa kutimuliwa tena bila mafao yoyote.
ReplyDeleteWanafukuzwa baada ya wabunge kuja juu. Ina maana waziri hakuona kabla mpaka wabunge walivyolalamika. Jambo hili limeripotiwa mda mrefu sana lakini hakuna hatua aliyochukua kuonesha mwendelezo wa kulindana. Tunaomba wanyama walioporwa warudishwe Tanzania.
ReplyDeletePolisi na Usalama wa taifa wanaona maandamano ya Chadema tu ila uporaji wa nchi ambao ni hatari kuliko hayo maandamano hawauoni. Shame on you guys.
Uncle acha kumezea post yangu. Wape waone hasara za kuuza hao wanyama nje ya nchi. Kama nilivyosema wazungu wanafungua mbuga za wanyama...mfano mzuri ni Safari Park ya San Diego, California-USA. Mpango wa wazungu ni kuwa miaka 50 ijayo hawana haja ya kuja Africa. Kama hamuamini angali hii link:
ReplyDeletehttp://www.sandiegozoo.org/park/plan_your_trip/hours_directions
Nawahakikishia wajukuu a vitukuu vyetu vitakula mawe. Tourism itaisha tu africa.....!! Uncle toa post yangu kuhusu hili. Mdau, California, USA
Hii nchi bwana wee acha tu, Wabunge wasingesema hao jamaa wangeendelea na kazi ya kusafirisha kama kawaida hao wanyama! Je ni kweli kwamba waziri alikuwa hajui au ameona aibu baada ya wabunge kulisemea?
ReplyDeletemdau swala hili la San Diego Maige analijuwa kweli?haya ndiyo yajayo na bahati mbaya hatunauwezo wa kuangalia zaidi ya kipindi cha nusu muongo.
ReplyDeleteKama kawa unda tume tu watu wale zaidi au sio bana.. Embu Maige na wenzako kueni serious yaani hamna njia nyingine za kuchunguza madai mpaka kila kukicha tume?? smfh!!
ReplyDeleteUncle, Asante kwa kutoa post yangu. Sasa labda niongeze kidogo. Mlima Kilimanjaro ambao ni mojawapo ya sababu kuwa ni kivutio cha watalii ni sababu ya kuwa na snow (Theluji) na upo katika nchi za tropic....kinachowavutia si urefu. Sasa kutokana na Global warming na hiyo theluji inayeyuka...maana yake ni kuwa hao watalii hawatakuja tena kenye mlima..sasa mkiuza na wanyama waje kufuata nini? Hivi mbona upeo wetu ni mdogo sana? Yaani kwaajili ya vijisenti tunauza nchi? Nawapa tena hii link kuwafungua macho. Hebu jamani tutumie hekima. Mdau-California, USA
ReplyDeleteMheshimiwa waziri mimi nilitegemea ungekuja na hukumu tayari juu ya hili swala bungeni,maana hili swala liko wazi kabisa hata mtoto mdogo anayeelewa maana ya neno "Nyara za serikali" anatambua huu ni wizi,isitoshe hili swala lilishazungumziwa kwenye vyombo vy habari kitambo na wewe ukasema uchunguzi unafanyika,unataka kuuambia umma wa watanzania katika huo uchunguzi umejitosheleza kiwango cha kuweza kuwasimamisha hao watendaji tena kwa malipo?! nani atakuwa anawalipa? na hao watakaokaimu watalipwa kwa fedha ipi? ya kodi zetu siye watanzania?
ReplyDeletewapi vyombo vya usalama? uwezo wenu ni wa kuwakamata wanaovunja maduka tu? ama wabeba unga?
" You can full some people for some times but not all the time "
Mdau Naunga mkono hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wezi wa mali za umma, ningependenda zaidi kuweka msistizo kwenye umakini katika kuhukumu pasipo uchunguzi wa kutosha, imekuwa ni kawaida kwa viongozi kuwachukulia wahusika adhabu kwa kukurupuka hasa baada msisimko wa umma baada ya tukio kutokea hii mara nyingi imesababisha watuhumiwa kushinda kesi because of missing some impontant links, kisha watuhumiwa hushitaki tena serikali na kulipwa pesa nyingi, vyombo vya uchunguzi havifanyi kazi vizuri, rushwa pia inakwamisha uchunguzi, ni heri watuhumiwa wawekwe ndani kwa kipindi cha uchunguzi, kwanza wanalipwa na wanapesa sijui mtawashinda vipi. Mwisho wa siku tunatengeneza vichwa vya habari magazetini siyo kukomesha uharifu.
ReplyDelete