Mohamed Raza ni Msanii Maarufu wa kimataifa ambaye ni hazina Halisi ya Taifu letu la Tanzania, alianza kazi yake ya sanaa za kuchora tokea enzi za Uhuru wa Tanganyika. Vizazi zaidi ya viwili vimenufanika na kuelimika kwa kusoma vitabu vyake tokea shule za msingi mpaka secondary hasa vya kiingereza kama familia ya Mr & Mrs Daudi na Mtakuja Primary School. Mbali na hapo Mzee Raza aliwahi kumchora Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Miaka ya 1960 na kufanikiwa kupata kazi katika chama cha TANU. Pia aliwahi kufaya kazi katika ubalozi wa Marekani Hapa Tanzania miaka ya 70.

Orodha haikuishia hapo aliendelea kuchora na kudesign stempu pamoja na nishani za mashujaa wa vita vya Kagera pamoja na kuwachora viongozi wengine wa serikali.

URBAN PULSE Ikishirikiana na Mwandishi Nguli wa habari Freddy Macha wanakuletea programme maalum ya Mzee Raza walipopata bahati ya kukutana nae hapa jijini London na kumdadisi kwa undani katika safari yake ya sanaa za michoro pamoja na changamoto mbalimbali zinazomkabili.

Wakati Tunaelekea katika Miaka 50 ya uhuru hatuna budi kukumbuka, kutambua na kumpatia heshima yake anayostahili kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika jamii yetu na ambaye ni Hazina ya taifa letu.

Programme hii itakuwa katika sehemu tatu, hivyo basi juinge nasi ili upate kumfahamu Mzee Raza kwa ukaribu zaidi,

Asanteni,
RAZA NA FRANK EYEMBE WA URBAN PULSE CREATIVE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huyu ndo jamaa aliyechora katuni za "chezo" ktk magazeti ya Daily news/Sunday News miaka ya 90? ingawaje nilikuwa sijui english,nilikuwa napenda kuangalia zile katuni.

    ReplyDelete
  2. FRANK UKO JUU, HONGERA endelea utafika tu

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza, sina hakika kama mzee Raza ndiye mchoraji wa "chezo" ila kitu ninachokijua ni kuwa Mzee huyu msanii alikuwa anachora picha za rangi tangu miaka ya 60 wakati wengi wetu ni watoto wadogo na wengine hawakuzaliwa. Pia najua yeye na (Paul?) Ndembo walichora stempu nyingi za posta enzi za Mwalimu (awamu ya kwanza). Je, kuna wadau ambao wanaweza kutueleza kama wasanii Mwaruko (wa Moshi) na Ndembo wako wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  4. Namkubali huyu mzee. Ni wasanii wachache sana Afrika wanaoweza kufanya kazi ya sanaa kuwa kipato chao kwa miaka hamsini! P. Ngowi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...