Home
Unlabelled
mzee pius msekwa ajibu tuhuma dhidi yake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Maelezo mazuri lakini wazee pumzikeni sasa jamani. Kila lenye mwanzo lina mwisho. Punzika kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
ReplyDeleteWe Anony wa kwanza unamwambia mzee wa watu apumzike kama baba wa taifa? In maana unataka afe? Kumwambia "achia ngazi" inatosha si mpaka useme "pumzika kama baba wa taifa".
ReplyDeleteNimeipenda hii ya "Neutral Obsever" mtandao wa gazeti la Mwananchi leo:
ReplyDeleteMsekwa: Nimetupiwa fitina inayoitwa usongombwingo
Comments
Neutral Observer 2011-08-23 11:16
Wataalam mnaojua mambo haya tafadhali nisaidieni kujibu maswali yafuatayo:
1. Utaratibu wa utoaji vibali kama hivi ukoje? Ni nani mwenye Mamlaka ya kuidhinisha na kutoa vibali vya ujenzi kwenye mbuga za wanyama? Waziri husika, Mkurugenzi wa Mamlaka, Mwenyekiti wa Bodi, Bodi nzima kupitia vikao, Wizara ya ardhi, Baraza la Mawaziri?
2. Waheshimiwa Wabunge walitoa vielelezo vya uthibitisho wa madai yao? Kama hakuna vielelezo je hii hatuwezi kuiita fitina au uzushi?
3.Je Msekwa ametoa majibu ya tuhuma dhidi yake kwa vielelezo vya uthibitisho?
3. Hizo za 5 stars zinazojengwa ni zipi na zinajengwa au zinatarajiwa kujengwa maeneo gani Ngorongoro?
4.Wakati wa harakati za ujenzi wa hoteli za 5 star Serengeti za Kempinski Bilila Lodge na Grumeti Lodge taarifa zake zilikuwa zinajulikana wazi kwa umma, ina maana kwa ngorongoro 5 star zinajengwa kwa siri hata NEMC na wanaharakati wa mazingira wamezibwa mdomo hawajatoa maoni yao? Hii kweli inawezekana kufanyika bila kujulikana katika generation hii ya kuscan na kuattach? Hata JF?
5. Je NEMC na wanaharakati wameshatoa kauli yoyote kuhusu jambo hili?
Ukiangalia mwelekeo wa maoni mengi hapa ni ule wa ushambulizi wa uzee na U-CCM wa Msekwa na siyo uchambuzi wa hoja alizotoa. Kwa kweli chuki dhidi ya CCM na serikali yake zimetufunika macho mpaka chochote kinachozungumzw a kutoka mdomoni mwa watu wao kinaonekana ni kama kinyesi tu wala hatujali kufanya uchambuzi wa kina. Tabia hii pia ipo kwa wapenzi wa CCM dhdi ya wapinzani. Wengi wetu tuna hulka ya kuchagua tu maneno tusiyoyapenda kutoka jedwali zima na kuyashikia bango kwa mashambulizi binafsi kwa mtoa hoja mradi tu ana mtizamo tofauti wa kisiasa. Huu ni ugonjwa mkubwa kwa watanzania ambao nafikiri unasababishwa na ubinafsi mkubwa uliyojaa kwenye nyoyo za baadhi ya jamii yetu. Inabidi tujitafakari kwa kina la sivyo hata mabadiliko ya uongozi wa Jamii hayatazaa matunda mazuri ya muda mrefu.
Wote hatupendi kinachoendelea lakini linapotokea jambo kama hili ni muhimu kuweka hisia zetu za kibinafsi na kisiasa pembeni na kujaribu kupata uthibitisho wa ukweli wa madai ya pande zote ili kupata taarifa sahihi za mgogoro huu vinginevyo tukiri kuwa tutakuwa tuneaendekeza majungu na fitina. "Trust but verify".
Hapa inaonekana mashambulizi mengi yanaelekezwa zaidi kwa mtoa hoja kuliko uchambuzi wa hoja zake. Huu ndiyo udahifu wetu wa kawaida.
Sisi vijana sasa hivi tupo katika harakati za kupokea hatma ya nchi yetu kutoka kwa hawa wazee wetu, tumeona makosa mengi yanafanyika na tunataka mwelekeo mpya lakini tujiulize kama miongoni mwa tabia zetu ni kuamini haraka taarifa au hoja zinazotolewa bila kuzitafutia uthibitisho na kujikita kwenye kushambulia watoa hoja kwa hisia binafsi na siyo kujadili hoja, Je sisi tutakapokuwa viongozi kesho hatutaendeleza tabia hii kwa wanaotoa hoja dhidi yetu?
Nitashukuru sana kama kama kuna mtu ataweza kusaida kujibu maswali haya kwa hoja na siyo kwa mashambulizi binafsi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Quote
Nimeipenda hii ya "Neutral Observer kwenye comments mtandao wa gazeti la mwananchi.