Mh. Anna Makinda (Spika)
Mh. Job Ndugai (Naibu Spika)
Taarifa ambayo imeibuka kuhusu Spika na Naibu Spika kutofautiana kuhusu maamuzi ya kuunda Kamati maalum ya kumchunguza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo si ya kweli.
Mh. Job Ndugai ameyaongea haya katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM cha leo na amekana huo ni uvumi tu wa watu ambao wasiolitakia mema taifa letu na wasioutakia mema ushirikiano wao mzuri ambao wanao yeye na Mh. Spika Anna Makinda, na vile vile Mh. Ndugai alilielezea pia uvumi ambao watu wameuzusha kuhusu yeye kuonekana ana nguvu zaidi ya Spika Anna Makinda;
Mh. Ndugai amekana hilo na kusema ni maneno tu yale yale! ambayo watu wasioutakia mema ushirikiano wao na kusema kwamba Mh. Spika Anna Makinda anamuamini sana na anamtuma katika shughuli nyingi tu ambazo ni muhimu lakini anaenda yeye Mh. Job Ndugai.
Clouds Fm walimuuliza maswali mawili matatu naye akayaongelea kwa ufasaha na kutaka wananchi waelewe hivyo anavyosema yeye, kuliko kusikiliza watu ambao wanazusha tu mambo ambayo sio mazuri.
Blog ya KAPINGAZ INAMPONGEZA KWA KUUELEZA UMA KWA UFASAHA ILI TUWEZE KUELEWA ZAIDI.
Michuzi tunaomba mtumie kiswahili vizuri mnapost habari kwani zinasomwa na watu wengi ambao miongoni mwao hutumia pia habari hizo kujifunza kiswahili (hasa wa nchi zisizozungumza kiswahili).
ReplyDeleteKichwa cha habari kina neno "MAHAMUZI" ambalo si neno halisi la kiswahili. Neno lenyewe ni MAAMUZI. Kuna watu wamekuwa wakiweka herufi H kwenye kwenye maneno enye herufi A E I O U. Wenye tatizo hili zaidi ni wahaya na jambo hili linakua siku hadi siku hata kwa watu waliozaliwa na kukulia mjini ambapo kiswahili huzungumzwa zaidi kuliko lugha zingine.
Mdau #1 si wewe tu uliyekerwa na tabia hiyo. Ipo pia tabia ya kukosea kosea maneno, mfano NENO...linaandikwa Nano na mengineyo mengi...halafu hawa-double check wanapost tu. Siku moja nlitoa maoni kwa nia njema tu nikiwa na hoja ya msingi km mdau ulivyosema kuwa Lugha yetu watu wengi wanajifunza..hivyo inasumbua sana, hata kwa natives tunapata shida kuona errors kama hizo. Ila Ankal ukaibania ile message yangu. Na ukibania hii nitakuhisi hutaki kusahihishwa na kujifunza wewe na timu yako. Kukumbushana ni kwa nia njema ya kujenga, kusaidia kizazi hiki na watoto wetu!
ReplyDeleteNdugai vipi mbona mbio kwenye vyombo vya habari? Kama yalosemwa ni uvumi si ukae kimya ukianza kujibishana kwenye vyombo vya habari that is weakness.Sometimes silence is the best answer.
ReplyDeleteMhhhh..! kuna kazi. Namuheshimu sana mama Anna Makinda kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa Taifa letu kwa muda mrefu ni kati ya Iron Ladies wa Tanzania.Lakini kwa kweli katika nafasi yake ya Uspika wa Bunge letu tukufu ninapata wasiwasi kama ni yeye kweli au anafanya makusudi kwa nia ya kuwafurahisha waliompa hiyo nafasi,YUKO "BIASED" sana na asiporekebisha utendaji wake wa kazi, kuliongoza Bunge kutamshinda amepwaya sana.Ndio maana watu wanaona kama naibu spika anamfunika.Hata hivyo naamini akimua kufanya kazi anayotakiwa kufanya spika wa bunge la vyama vingi anaweza, muda bado ni mrefu natumaini atajirekebisha, umma wa watanzania wanaona kila kitu bungeni na wana akili sana hata kama hawako mjengoni.
ReplyDeleteJairo atawamaliza, yule ni mafia wa siku nyingi. Hii issue isipoangaliwa italeta balaa Tanzania.
ReplyDeleteHii society ni male chauvinistic. Mwanamke hata afanye vipi watu wanaassess vibaya. Tatizo ni kwamba sio kama sitta aliekuwa anapenda kuwaruhusu watu wenye majungu watoe tope zao bungeni, yeye hana hilo ndio anaonekana biased. Keep it up mummy, hii ni reflection ya society yetu na ndio yanayowakuta wanawake wote humu makazini kwetu. Tena afadhali ya wewe sisi wavaa mitandio ndio kabisa. Mtu anakuuliza where did you learn your english, you speak very good english. Ala !!!!!!!!! there is this attitude towards women.
ReplyDeleteMheshimiwa Ndungai kwa maoni yangu binafsi nadhani kusema ni jambo jema. Kwanza inakupa unafuu wewe mwenyewe, na pili inaweka mambo wazi kwa upande wa pili (mwingine). Kitu cha msingi au cha kuzingatia sana ni jinsi utakavyotoa maoni yako, au kauli. Maana neno baya ni baya, lakini neno zuri linaweza kuharibiwa na sauti ya mtu mwenyewe.
ReplyDeleteHata hivyo ninakuomba utafute busara zaidi, maana taifa linakuhitaji kwa miaka mingi ijayo.