Nnauye akiagana na ujumbeuo
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) akizungumza, wakati ujumbe wake ulipokutana na ujumbe wa kutoka Kituo cha Demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini Malawi (kushoto) katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam leo. Ujumbe huo umeongozwa na Mwenyekiti wa kituo hicho, Levison Ganisa (wanne walioketi). Wenyeji wa ujumbe huo ni Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).Kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu, Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.Picha na Bashir Nkoromo.
Home
Unlabelled
NNAUYE AKUTANA NA UJUMBE WA MALAWI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Jamani hivi huyu jamaa ni nani?kuna nini kinakuja kutoka kwa huyu jamaa,maana kila leo ofisi hii kesho ile, kwani si-si-e-mu hakuna kazi zingine za kujenga nchi ila ni kutembelea vituo mbalix2 na kutembelewa tu.
ReplyDeleteNchi ipo kwenye shida nyingi sasa ,ni wakati wa kurudisha imani ya wananchi na sio mda wa matembezi yasio na faida kwa wananchi.
Mzee si utembelee Sinza kwenye shida za mafuta ukakutane na ujumbe wa walalahoi waliopanga foleni ya mafuta na wanaohitaji maelezo kutoka viongozi wao.
ReplyDeleteMichuzi team, naomba swali langu liwekwe hapa.
ReplyDeleteJe, Nape anaandaliwa kuwa candidate wa CCM katika uchaguzi ujao au vipi? Mbona matokeo mengi yake kikazi yanaanikwa hapa? Tujulisheni basi, tuweze kuhoji...
Mdau wa kwanza acha chuki binafsi, kwani Nape wewe anakuhusuje, akiwa Rais wananchi watakuwa wamempa urais...mbona unakuwa km hujakomaa wewe! Kwani Anko Ankal analeta matukio ya Nape peke yake? Mbona tunayaona kuanzia ya Rais na viongozi wengine wowote. Simtetei Nape lakini nacritique pointless yake ya kumtaka kumjua Nape, hoja yako haina mashiko!
ReplyDeleteHata wadau waliotangulia pia hawakuonyesha point yeyote ya maana,matatizo ya nchi na maendeleo ni jambo moja lakini kukutana na wageni pia na kuwapa maelezo na kubadilishana fikra ni sehemu ya kazi yake,...mara ngapi ametembelea watu wenye matatizo?hata akifanya jambo gani kwenu ni baya tu,labda mngesikia habari za akina PADRI SLAA ndio mngeshangilia hata kama sio cha maana.
ReplyDelete