MBUNGE WA JIMBO LA KITOPE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA AMBAYE PIA NI MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. BALOZI SEIF ALI IDDI AKIWAHUTUBIA MABALOZI WA NYUMBA KUMI WA NDANI YA JIMBO LAKE, BALOZI SEIF AMEFANYA ZIARA YA KUKUTANA NA MABALOZI HAO KWA LENGO LA KUKIIMARISHA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitosita kuwachukulia hatua za kisheria muda si mrefu viongozi wote waliohusika na masuala ya uvushaji wa magendo ya zao la karafuu nje ya Nchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mabalozi wa CCM wa Mashina yaliyomo ndani ya Wadi ya Fujoni hapo Afisi ya CCM Tawi la Fujoni Wilaya ya Kaskazini B.

Balozi Seif amesema Viongozi waliohusika na Biashara hiyo ya Magendo ya Karafuu wanajuilikana na hatua ya kuwachukula sheria ina lengo la Kulinda Heshima ya Serikali.

Amesema uamuzi wa Serikali wa kupandisha bei ni kuimarisha pamoja na kushajiisha uzalishaji wa zao hilo ambalo ni uchumi na muhimili wa Uchumi wa Taifa.

“Hakuna sababu tena ya zao la Karafuu kuuzwa nje ya Nchi Kimagendo kwa vile bei ya bidhaa hiyo imepandishwa kuzingatia soko la Dunia ” . Alisema Balozi Seif Ali Iddi.

Amewaomba wakulima kuzidi kuimarisha kwa wingi uzalishaji wa mikarafuu mipya kwa lengo la kujiongezea kipato chao na kupunguza makali ya maisha.

Akizungumzia suala la uchaguzi wa Viongozi wa CCM utakaofanyika Hapo mwakani Balozi Seif ambae pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM amewatahadharisha Mabalozi hao kuwa makini katika kuepuka tabia ya kutanguliza ujomba katika kuchagua Viongozi.

Balozi Seif amesema ni vyema ikaeleweka kwamba wanayemchagua anafaa kuwaongoza akiwa na vigezo vyote vya uongozi.

Amesisitiza kwamba Tabia ya kuendeleza urafiki katika suala la uongozi inapunguza sana nguvu za chama.

Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kitope amemaliza ziara yake ya kukutana na Mabalozi wa Mashina ndani ya Jimbo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...