Na Idara ya Habari (MAELEZO),Zanzibar
Hatimaye mafundi wa Shirika la Umeme Zanzibar wamekamilisha matengenezo ya transfoma katika Kituo cha kupokelea umeme Mtoni Kisiwani Unguja.
Ofisa Uhusiano wa ZECO, Salum Abdallah amesema transfoma hilo liliharibika mwishoni mwa wiki ambapo mafundi wa Shirika hilo walifanya jitihada maalum kukamilisha matengenezo kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu wananchi.
Amesema kwamba kazi ya kutengenezo trasnfoma hiyo ilifanywa kwa pamoja na mafundi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) ambapo kazi hiyo ilimazika jana usiku na huduma ya umeme kurejea katika hali ya kawaida.
Amesema baada ya kukamilika kwa matengenezo hayo, mgao wa dharura uliokuwa ukidumu kwa saa zaidi ya moja sasa umemalizika na utaratibu wa kawaida utaendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...