Asalaam Aleikum Kaka Michuzi,
natumaini wewe ni mzima wa Afya. Mimi naitwa Mussa Ally and i made a short film inayo husu hasa wale wasanii wa kwanza kuingia kwenye Hip hop Tanzania..nime itengeneza hii video kwa madhumuni makubwa ya kwa wale wasio faham kiundani zaidi kua Hip Hop ina tokea wapi na ina elekea wapi,na hii Ideer niliipata baada ya kusoma Topic moja kubwa sana kutokea kwenye Blog yako na nilivyo soma zile comment nikaona mabishano makubwa sana na nadhani itakua vizuri sana na pia nita shukuru sana kama itawezekana kwa Michuzi Blog kui Post hii video ili mashabiki wa hip hop pia wasanii iwa weze kuiona hii Video .
Asante Kwa mara nyingine Bwana Isaa Michuzi na Link zote nime Ziandika hapo Chini.


Binafsi naona kabisa Saleh jabil ndiye alikuwa wa kwanza kurekodi tapes na kuziingiza mtaani watu tukanunua japo alikuwa akirudia kile kilichoimbwa na wasanii wa ulaya na America kwa kubadili mtiriliko wa sauti katika lugha ya kiswahili. ilikuwa ni kipindi ambacho vijana haswa kwenye shule za sekondari walivutwa sana na upepo wa saleh Jabil, namkumbuka sana na mpaka leo nina tape yake nyimbo kama Ice Ice bby wa Vanila Ice, hip hop hurray wa naughty by nature bila kusahau OPP. kwa yeye kufanya vile baadae ndo walianza kuibuka wengine. siyo rahisi kutenganisha mwamzo wa bongo fleva bila saleh jabil
ReplyDeleteTHE RECORD IS NOW STRAIGHT. IF U DISPUTE MAKE YOUR VIDEO LIKE THIS.
ReplyDeleteOK,nimefuatilia clips zako,mimi ni mmoja aliyekuwa ana rap miaka ya mwisho ya tisini ila kutokana na music kutokuwa real nikaamua kwenda shule tu,anyway point yangu hapa una idea muziki wa hip hop bongo ulitokea wapi ila kuna mapengo mengi yanaonekana kwenye clips zako...kwanza unajua kuna wasanii wengi sana,walikuwepo miaka ya 80 na 90 ambao walichangia huu mziki ila hawakuwahi kurekodi simply kwa sababu ya fedha na uhaba wa studio na kuna wengine wamerekodi ila sijui kwa nini umewasahau.nitakupa list yao kidogo..nashangaa umewasahau watu kama kina soggy,unique sisters...unajua witney wa wakilisha watu wanajua alitoka kipindi cha coca cola pop star ila witney ni mmoja wa wanamuziki wanawake waliokuwepo toka miaka ya mwanzo ya 90..anyways check hii list
ReplyDelete-N2P-niggaz 2 public
-da young mob
-BDP-big dog pose
-BGZ-blackgansterz(humu kulikuwepo kina TID,ambaye wengine wanajua anaimba ila ukweli TID ni rapper mzuri sana,naye alianza miaka ya 90,watu hawajui hilo)
-mob in genious(humu kuna mtoto mmoja wa kisomali wanamuita aidid na mwenzake jina limenitoka)
-KIBO FLAVA
-LYRICAL GENIOUS
-MC CHIVALO
-MALIK
DA WAPO WENGI SANA KUNA HAJA YA KUWATAFUTA HAWA WOTE NDIO UTAPATA HISTORY NZURI SANA.
good idea ila kama mdau alivyosema kwamba kuna watu ama makundi kibao umeyaacha, siku laumu kwa sababu tatizo letu kubwa liko kwenye documentation, ungefanya utafiti zaidi ingekuwa poa mno, ni kweli anony wa juu hapo anavyosema kuna artists kibao ambao watu wanadhani ni wajuzi like Witness ni wa long-time kabla hata ya ZayB, Sister P ama Dataz!!!!! kingine mzee documentary yako haina mtiririko mzuri kwa sababu unakuta makundi yale ya mwanzo unaweka mwisho kitu kinacho poteza maana, Diplomats was my favorite group by then, the only studio was DonBosco kwa Kaka Marlon! Big up lakini kaka kazi nzuri angalau umeanzisha na hatupaswi kuchonga sana kama tunajua sana!
ReplyDeleteAsaalam Aleikum ni Mussa Ally hapa
ReplyDeleteOkey nime wasoma na Asanteni sana kwa maoni yenu mliyo ya toa mpaka sasa na Pia Niko Na Big Plan (Big Project) ya Documentary itakayo fwatia Kuhuusu Hip Hop yani hii Hapa ilikua ni simple kama mlivyo iona na ningependa zaidi kusema kwamba kwa wale ambao mna kumbu kumbu nzuri List kama hizo majina makundi na pia History kwa umbali naziitaji ili niweze kutengeneza Documenatary moja ambayo itakayo kubalika kwa kila mtu na Kwa maoni zaidi maswali usisite kutuma mail kupitia
mussaally@hotamil.com
Asanteni sana!!
Musa nikupe hongera kwa idea uliyokuja nayo ni nzuri kwa ushauri tu ujaribu kuwasiliana na blog za kama Arusha, Mbeya, Mwanza, Dom na mikoa mingine nakumbuka kuna vichwa vilikuwa vinatokea mikoani vipindi vya likizo mwanzoni mwa 1990s vilikuwa vizuri lakini ukosefu wa promo uliwakatisha tamaa. Bila kumsahau Dogo Mwendawazimu Hashim alikuwa UDSM miaka ya 2007 mtafute ayakujuza mengi ongea na Bon Luv na group lakina Kim, Saigon
ReplyDeleteMZEE UMEMSAHAU MTU MMOJA WA MID 90'S ANAITWA SOS B WA MA B(MABIBO) DUDE HAD REALLY SMOOTH FLOW( SNOOP LIKE).KIPINDI CHA SALEHE JABILL, KUNA ALBUM, NYINGINE YA WEUSI WAGUMU ASILIA(SOGGY AND HIS CREW)."CHOKO CHOKO MCHOKOE PWEZA BINADAMU HUTOMWEZA..."
ReplyDeleteSafi sana , lakini mbona sijawasikia Diplomatz kwenye clip zako? Kina Salehe na wenzake wa Diplomatz ? Lakini safi sana.
ReplyDeleteMdau Texas.
Albam ya Swahili Rap ya Saleh Jabil ilitoka 1991. Kulikuwa hakuna kundi lolote la Hip Hop lilikuwa linasikika kipindi hicho. Makundi yalianza au yalianza kusikika mwaka 1993 ikiwemo Kwanza Unit. Hip Hop ilipata umaarufu kuanzia mwaka 1994 ilipoanzishwa ITV na Radio One ndipo jamii ilipoanza kusikia na kuwa karibu na Hip Hop. Na hapo ndipo makundi mengi yalisikika nakuanza kujulikana.
ReplyDeleteKikingine ambacho inabidi mkikumbuke ni kuwa makundi yote ya mwanzo na waimbaji wa mwanzo walikuwa wanatumia kiingereza, hili ilifanya hip hop kuwa ni ya watu aina fulani.