Timu nzima ya Globu ya Jamii inafuatilia kwa ukaribu habari za kimbunga Irene ambacho tunaambiwa kitashambulia sehemu kadhaa za Marekani katika masaa 24 yajayo. Tunajua miji yote husika ina wadau kibao, hususan ndugu zetu toka Tanzania. Tunatoa pole na pia kuuliza kama ndugu zetu mko salama???
Tunawatakia kila la heri na Mola awalinde
-Michuzi
ANKAL,ASANTE SANA KWE KUTUCHUNGULIA KAMA TUPO SALAMA.HIVI SASA MWENGE (TROPICAPICA STORM IRENE)ULISHAONDOKA NORTH CAROLINA UNAELEKEA VIRGINIA. ACCORDING TO CNN MWENGE UMEUA MTU MMOJA (SIYO MTANZANIA) KULE NORTH CAROLINA.HAPA DC TUTAUPOKEA MAJIRA YA SAA MBILI USIKU AMBAYO NI SAWA NA SAA TISA ALFAJIRI HUKO NYUMNANI.KWA SASA NJE KUMENUNA,GIZA LIMEAMBATANA NA MVUA TUNATUMAINI UTAPITA SALAMA ILI TUUKABIDHI KWA WENZETU WA DELAWARE ILI NA WAO WAWAKABIDHI WENZETU WA KASKAZINI. STAY TUNED KAMA UMEME HAUTAKATIKA. WATANZANIA TUPO SALAMA KWA SASA
ReplyDeleteMzee Mithupu , pole na "swaumu" watu wapo salama mungu anasaidia. Mimi nina swali la Kizushi , kwanini hivi Vimbunga vyote vya hili taifa (STATES) vinapewaga majina ya Kichaga? sasa ni Iren, vilivyopita Ritta, Makdalena....etc! ukiweza lirushe hili swali la kizushi hewani.
ReplyDeleteMKUU WA LIBENEKE, IRENE AMESHAUA WATU WANANE HADI SASA (SIYO WATANZANIA). KAINGIA VIRGINIA BAADA YA KULIPUA NORTH CAROLINA. DC TUPO MKAO WA KULA. KWAVILE WATU MILIONI NANE HAWANA UMEME MPAKA SASA, HATUNA UKAKIKA WA KUENDELEA KU- ACCESS LIBENEKE.
ReplyDeleteIrene ashapitia hapa kwetu bila kutuwacha katika hali yenye uharibifu mwingi. Tushapoa hasa baada ya kuepuka chupuchupu hapa kwetu katika eneo la magharibi mwa Virginia. Ila ni mteteko wa hapo Alhamisi uliyo sababisha uharibifu mwingi nyumbani kwetu. Marekebisho yataendelea kwanzia mnano Jumatatu na kumalizika hapo Ijumaa. Jambo lenye uchungu mwingi kwetu ni kwamba tulikua bila bima ya mtetemeko, kwa hivyo tutavumilia kikondo. (We will bite the bullet and be able to come home during the December end year holidays. Thanks for your concern).
ReplyDeleteMdau.
(Great Falls,
Virginia).
Tuko Salama Mkuu: Mvua bado Inamiminika hapa DC na Upepo mkali: 5 deaths so far.
ReplyDeleteMdau wa majina ya vimbunga umesahau na Katarina! Hivi nani anakumbuka tulivyokuwa tunaimba tulipokuwa wadogo "mvua njoo, Katarina njoo" kumbe tulikuwa tunaita mvua ije na kumbunga kikubwa bila kujua!
ReplyDeleteRefer to Malthus theories on Google.
ReplyDelete