Mbunge wa Tabora mjini na Mwenyekiti wa Simba SC Ismail Aden Rage akiongea na simu nje ya ukumbi wa Pius Msekwa wa  jengo la bunge mjini Dodoma leo. Rage kaiambia Globu ya Jamii leo kwamba Spika Anne Makinda ameialika timu ya Simba kupeleka Ngao yao ya Jamii waliyoipata kwa kuwafunga watani wa Jadi Yanga bao 2-0. Pia Rage amesema wekundu hao wa Msimbazi wamevunja mikataba ya wachezaji wawili Eric toka Uganda na Ocheing wa Kenya ili kufanya idadi ya  wachezaji wa nje wa kulipwa iwe tano kama kanuni za TFF zinavyoainisha. Kasema Eric ameondolewa kikosini baada ya kupata majeraha yatayomfanya asicheze kwa miezi minne na Ocheing amekatwa kwa sababu uhamisho wake wa kimataifa haujakamilika na ligi ndio imeshaanza. Kivazi cha siku isiyo rasmi ya kikao cha bunge huwa ya kawaida
 Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mh Samwel Sitta, ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki, akiongea na mwanahabari wa TBC1 Jane Mosha baada ya kumalizika kwa semina ya siku moja kwa wabunge juu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
 Baadhi ya wabunge wakitoka mjengoni baada ya semina ya Wizara ya Ushirikiano wa Jumjuiya ya Afrika Mashariki
 Mama Margareth Sitta mbunge wa viti maalumu CCM (shoto) Ismail Aden Rage na Bi Leticia Nyerere (viti maalumu- CHADEMA) wakitoka mjengoni leo
Wabunge wakibadilishana mawazo baada ya semina hiyo
Waheshimiwa wabunge wa mkoa wa Tabora kwa tiketi ya CCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana leo mjini Dodoma kupanga mikakati ya maendeleo ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa Igunga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Comment moja tu: Nimeipenda shati la Mh. Sitta.

    ReplyDelete
  2. Ankal, Wasomaji wengi hatutoki Tabora. Angalau ungeliweka caption yenye majina ya hao wabunge.

    ReplyDelete
  3. MUHESHIMIWA RAGE MBONA UMETINGA KI CHADEMA CHADEMA,KUVAA SARE ZA CHAMA CHAKO HIMANANISHI WEWE NI KWALA AMAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Ninyi watoa maoni hamuelewi. Hamjui kama Rage na Mheshimiwa 6 ni wapenzi wa Simba? Hapo wana furaha kupita kiasi baada ya simba kumfumga Yanga juzi. Alichovaa Rage sio scuf ya CHADEMA ila ni ya Simba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...