Habari Ankal,

Ninapenda kuandika mada yangu kwa huzuni wa uchafu na wizi uliokithiri wa vipaseli/mizigo ya waungwana wasio na hatia kwenye shirika posta. 

Mbali na ukweli kwamba, watu mbali mbali hasa walioko nje ya nchi, hulipa kodi pande zote, yaani Ulaya na kulipia tena asilimia karibu 50 ya vitu hivyo vikifika Dar, Bado wafanyakazi wa Posta wanakuwa na ujasiri wa kijinga wa kuiba mizigo hiyo.

 Nikisema kuiba mizigo hiyo, ina maana wanafungua mizigo kabla ya mizigo hiyo kuwafikia wahusika. Wanachambua vitu vyenye dhamani, kuviiba, halafu kujifanya hawajui nini kinaendelea. Wanatupiana Lawama eti, ohh.. huu mzigo umepitia kwenye kitengo cha mizigo ya ulaya na uchafu kama huo.

Tendo hilo linasikitisha sana na linachefua, kwani watu mbali mbali wanaotuma vijimizigo kwa ajili ya ndugu zao, wanakuwa wanatenda lililo la haki. Uongozi wa Posta hauna budi kuweka mikakati maalumu na kuwadhibiti wafanyakazi wa Posta walio na dhiki ya kufa. 

Ninasema hivi kwa uchungu kwani hii ni mara ya tatu, natuma mizigo kutoka Marekani kupitia Posta, na mizogo hiyo kufunguliwa kabla ya kuwafikia wahusika. 

Hao wafanyakazi wa Posta wenye uwezo wa kusoma kilichoandikwa juu ya mizogo hiyo, na wakijua ni kitu chenye dhamani, basi hufungua, na kuchukua vitu vyenye Dhamani, na kubakiza visivyo na dhamani sana. Hii ikimaanisha hata kujifanya wanarudishia kufunga mzigo huo.

Tafadhali watu wanaohusika na wizi wa Mizigo, Posta Acheni tabia hizo chafu. Mnalipwa mishahara, na inabidi muheshimu kazi zenu. Kuna watu wanaotafuta kazi kama hiyo, na wana uwezo wa kuhakikisha uaminifu.

Shukrani Kaka..

Mdau Gallus

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Wizi wa mizigo ni tatizo sugu. Hususan TZ. Lakini pia mimi niliwahi kuleta mzigo ambao mpaka hii leo unaniuma sana. Wakati nipo UK nilituma mzigo ambao kulikuwa na hi-fi zile za piece na nilichukua brand tofauti. Ajabu ni kuwa piece ya CD iliibiwa pamoja na cable moja ya speaker ambayo ilikuwa inatoa sauti safi kabisa. Sikufurahiya hicho kitendo. Nilipofuatilia kwa kampuni ya DEWJI, niligundua kuwa waliiba kule kule UK na kwenye hii kampuni ya DEWJI. Huyu jamaa nilipolalamika anilipe akadai nimpe risiti za TRA. Sasa ujanja aliotumia hakuandika vitu vyangu kimoja kimoja bali aliandika "Personal effect" sasa TRA nao wakanipa risiti ya "Personal effect". Sasa akanishinda huyu DEWJI na sikupata malipo yangu mpaka leo. Kwa ufupi ninachotaka kusema ni kuwa wakati mwengine vitu huwa vinaibiwa ughaibuni kabla ya kufika TZ. Uwanja wa ndenge wa Heathrow unaongoza kwa wizi wa mizigo, cha ajabu kuwa waliokamatwa wote ni wazungu!

    ReplyDelete
  2. pole sana kaka wizi wa wafanyakazi wa posta hautaisha kwa wewe kutuma malalamiko yako humu ktk michuzi. USHAURI WANGU NENDA KAIOMBE POSTA YA HUKO U.S.A MAHALA ULIPO WEWE UTUME TENA KIFURUSHI CHENYE DHAMANI KUBWA ZAIDI YA HIVYO VILIVYOIBIWA HALAFU MFUNGA KIJICAMERA (MTEGO) ILI MUWAKAMATE WALE WEZI KULE BONGO HAPO NDIYO UTAPUNGUZA WIZI WA BONGO MANENO NI MANENO TU FANYENI VITENDO MBONA HILI NI JAMBO DOGO SANA JAMANI KWA NCHI ZILIZOENDELEA.

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu Gallus pole sana, sasa usijaribu kutuma barua kwenda kwenye banki yoyote Tanzania hata kama ni barua tu ya kawaida itafunguliwa na kutupwa. Nimesha wahi kutuma registered mail nimeifuatilia mpaka nimekoma, imetua Tanzania ndiyo ikayeyuka ni miaka kama saba hivi sasa. Naona hapa lazima viongozi wanashiriki kwenye hili, haiwezekani wanaohujumu shirika wasijulikane. Kama hakuna kiongozi anayelimudu hili, wanipe mimi hilo shirika kwa ujinga wangu walao mwezi mmoja tuone kama kuna kitu kitapotea. Kila mtu anajua jukumu lake kwanini wasikamatwe? Uozo tu wa shirika hakuna jingine. Degelavita.

    ReplyDelete
  4. Mangi wa KiboshoAugust 05, 2011

    My Dog! hadi leo unatuma mzigo kupitia Posta? Wafanyakazi wake umewaona walivyo? ni the chokest kwa sana! mishahara ni ile ile ya mwaka 47! kuipata pia ni kwa mbinde mwanawane! Ukome na ukomae! Ebo!

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni wa kwanza unatatanisha na mara Heathrow, mara kampuni ya Dewji mara wazungu wamekamatwa..hueleweki mdau!

    Lakini pia tusiwe wepesi wa kuwahukumu posta Bongo bila kuwa na ushahidi kuwa huo wizi umefanyika hapo posta. Kama mzigo umekuwa documented ipasavyo, nini kilichomo na thamani yake ni rahisi kufuatilia, kwani posta nyingi za ulaya wanaguarantee kukufikishia mzigo wako. Kama ukipotea wanalipa thamani ya mzigo ulio potea. Tatizo letu ni kwamba tunaandika uongo. Mtu unatuma kitu kipya cha 5M unaandika Personal effect, ili ulipie $20 shipping na Bongo usilipie kodi TRA. Mtu akiona si atavutiwa, na ushahidi hakuna. Hapo aliyeuza kauza dhahabu feki na mnunuzi pia kalipa kwa fedha feki, ngoma droo!

    Binafsi nimetuma vitu vya thamani kubwa tu kwa njia ya posta kutoka ulaya, na vimefika salama u salimini. Huu sio utetezi kwa kampuni ya posta Tanzania.

    ReplyDelete
  6. Kwakweli hata mimi niliacha kutuma mizigo sbb kwanza wanatutoza tena ushuru mkubwa inakuwa kilekitu unakinunua mara tatu yake na ni personal efect!Na swala la wizi kweli U.k kuna wizi sana upande wa posta walitowa mpaka kwenye ma tv!lakini na tanzania wanatukomoa sana sisi tuliokuwa nje
    kutulipisha maushuru yasiokuwa na kichwa wala miguu!nimeacha kutuma chochote!sasa wao ndio wanapunguza mapato kwa tamaa yao ya fisi!

    ReplyDelete
  7. MDAU wa KWANZA naona UONGO umekukamata watu wanaongelea POSTA wewe umekazania DEWJI, sijui Heathrow Vitu tofauti mambo ya mizigo ya Cargo na anavyoongelea mdau ni kutuma kutoka nje kwa POsta kufikia Posta sio mambo yale ya cargo mtu anakopoa Nje na Huku Bandarini vitu tofauti wacha kubabaisha utakuta huyu aliyeandika ni mtu wa POSTA ya TANZANIA anajisafisha hapo lol! ila kama Mdau mmoja kaongea unaweza kwenda pia Posta ya Ulaya ukalalamika vitu vilivyokuwepo vimepatikana nusu wakatizama wapi kulikuwa na tatizo. TABIA ZA TAMAA WACHENI ALAFU MNARUDI MAKWENU OH WIFE NIMEKUNUNULIA HII KITU AU MWANANGU AU FAMILIA YOYOTE HAMNA AIBU JAMANI HAMUMUOGOPI MUNGU? KZ

    ReplyDelete
  8. Wacha kutudanganya wewe. unawasingizia wafanyakazi wa posta Tanzania bure tu. kumbuka huko unapotuma kifurushi kwanza wanakiscan kabla ya kukipandisha kwenye ndege na wakiona vitu visivyo kawaida wanafungua na wao wana tamaa hivyo wanakwiba kwa kujua kuwa lazima utawasingizia wabongo wenzako.
    kwa nini usitume kwa dhl ambapo utafunga mbele yao na utaorodhesha kila kitu? unaogopa gharama?

    ReplyDelete
  9. jamani mi nona porojo tu kiukweli halisia ni kuwa kweli posta ya tanzania ni wezi simaanishi wote la hasha, ila kama walivyosema waungwana wawili watatu hapo juu kwamba ukiipoteza mzigo wako. na ukiwaambia poata mfano ya uk huwa wanakuwa na kitu kina itwa parcel track number wakiingiza nanmba kwenye systems zaowatakwambia mzigo umefika tanzania lini na saa ngapi.. ila ukiwaambiwa mtu wako hajaupokea unawapa risiti na wanakurudishia pesa yako japokuwa muda mwingine ni process ndefu... laiza ndo maana kuna posta na dhl kama uwezo wako dhl mshukuru mungu na kuna wengine wanaona dhl gharama.

    ReplyDelete
  10. kwa Dewji London kuna CCTV kila kona, kila hatua ndani ya ghala mpaka nje ya ghala, hivyo mfanyakazi wa Dewji London kuondoka na kitu siyo kirahisi hivyo.

    Dawa ni sehemu zote ambazo zinapokea mizigo DSM kama POSTA, AIRPORT, Bandarini n.k CCTV ziwekwe kila kona na kila kichochoro cha eneo la shirika hapo Tanzania. Mtu akikwapua kitu au akionekana anafanya mambo ya ajabu mambo yote yatakuwa hadharani ktk hifafhi za clips za CCTV.

    Mdau
    Jijini London.

    ReplyDelete
  11. Vitengo vyote vinavyohusika na mizigo vimejaa wezi. Usiombe utue bongo halafu mzigo wako ufike na ndege nyingine, wale jamaa wa swissport wanabomoa kufuli, wanaiba, na kurudishia kufuli jingine, kisha wanakutafuta na kukuletea mizigo yako. Kama muvi vile, japo unaweza kumuua anayekuletea huo mzigo.

    ReplyDelete
  12. PRETTY SINTAH BLOG IKO JUU KAMA ANKALIIIIIIII

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...