Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia
Dkt. Augustine Mahiga
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augstine Mahiga amesema wahenga hawakukosea kunena "atafutaye hachoki, akichoka keshapata", akiuelekeza msemo huo kwa juhudi za kusaka amani ya kudumu nchini Somalia suala ambalo limekuwa likiendelea tangu kuangushwa kwa utawala wa Siad Barre miaka zaidi ya 20 iliyopita. 

Wiki hii amelifahamisha baraza la usalama juhudi za jumuiya ya kimataifa na hususan Umoja wa mataifa zimeanza kuzaa matunda Somalia, kwanza kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al-Shabaab limefungasha virago na kukimbia Moghadishu, pili Rais na Spika wa Bunge waliokuwa na mfarakano kwa muda sasa wameshikana mkono na zaidi ya hapo wako tayari kumalizika kipindi cha serikali ya mpito na kufungua ukurasa mpya katika amani ya kudumu ya Somalia. Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa,Flora Nducha ameketi na balozi Magiha kujadili hatua hizo. Wasikilize kupitia

AU
AU
AU moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...