Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali duniani hapa Canada wamefika katika Ubalozi wa Tanzania,Ottawa kusaini katika kitabu cha maombolezo kufuatia msiba mkubwa uliolikumba Taifa la Tanzania kufuatia kuzama kwa meli ya MV Spice Islander katika mkondo wa Nungwi, Zanzibar.
Balozi wa Burkina Faso nchini Canada,Mhe.Juliette Bonkoungou akiweka saini kitabu cha maombolezo ya waliopata ajali ya Meli ya Mv. Spice Islander iliyotokea hivi karibuni huko Zanzibar.
Mke wa Balozi wa Canada nchini Tanzania nae alifika Kwenye Ubalozi wa Tanzania na kutia saini kwenye kitabu cha Maombolezo ya waliopata ajali ya meli huko Zanzibat,Tanzania.
Mkuu wa Itifaki kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada, Bibi Margaret Huber akiweka saini kitabu cha Maombolezo ya waliopata ajali ya meli huko Zanzibar,Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...