Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini ( TAKUKURU), Dk Edward Hoseah,( aliyesimama) akifafanua jambo kuhusu msingi wa kujitegemea  mbele ya wahitimu watarajiwa wa kidato cha nne kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Serikali Mzumbe, ( hawapo pichani) Wilayani Mvomero, Mkoani Morogoro, wakati  mahafali ya 51 ya Shule hiyo juzi kwenye ukumbi wa shule hiyo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Serikali ya Mzumbe , Pascal Kihanga  (kulia) akitoa shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini ( TAKUKURU), Dk Edward Hoseah,( watatu kutoka kushoto walioketi )ambaye juzi alikuwa mgeni rasmi katika  mahafali ya 51 ya kidato cha nne ya  wahitimu watarajia wa Shule ya Sekondari ya Serikali Mzumbe,  Wilayani Mvomero, Mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), Dk Edward Hoseah,akimshika mkono mmoja wa wanafunzi wa klabu ya wapigavita rushwa wa  shule ya Sekondari ya Serikali ya Mzumbe, iliyopo Mkoani Morogoro   baada ya kukabidhi  zawadi ya seti ya Kompyuta kwa ajili ya matumzi ya Klabu hiyo wakati wa mahafali ya wahitimu watarajiwa wa kidato cha nne  kwenye  mahafali ya 51 ya Shule hiyo yaliyofanyika Septemba 15, mwaka huu.
 Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), Dk Edward Hoseah, akimkabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya Sekondari  kidato cha nne  ,mtarajiwa Claude Kunze , wa shule ya Sekondari ya Serikali Mzumbe iliyopo katika Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, juzi  wakati  wa mahafali ya 51 ya Shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo.
Baadhi ya wahitimu watarajiwa wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Serikali Mzumbe, Mkoani Morogoro wakimsikiliza mgeni rasmi, Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini ( TAKUKURU), Dk Edward Hoseah, ( hayupo pichani), wakati  wa mahafali ya 51 ya Shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo Septemba 15, mwaka huu.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...