Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa Tanzania na sasa Afrika Mashariki na penginepo duniani atakuwa mmojawapo wa wahudumu wa semina na ‘conference’ itakayofanyika College Park, Maryland Marekani kati ya tarehe 3 - 9 Oktoba 2011. Kwa habari zaidi kuhusu huduma hiyo tafadhali tembelea hapa: http://thewayofthecrossgospelministries.org/upcoming-events-page
Christina Shusho ametoa albam mbili mwaka huu 2011 zijulikanazo kama ‘Nipe Macho’ na ‘Kwa la Kanisa Kristo’ na zinapatikana kwa viwango vya audio (CD). Kwa wale walioko Marekani na Canada inawezekana wakapata Video za mojawapo ya albamu hizo wakati wa ziara hii kama zitakuwa zimekamilika.
Christina Shusho ni mtumishi wa Mungu na amekuwa baraka sana popote alipohudumia. Kwa hiyo Marekani na Canada kaeni tayari kupokea baraka zako wakati wa conference hii. Inawezekana kabisa akatembelea pia state nyingine kama Texas (Houston na Dallas). Hii haijahakikishwa, mtafahamishwa habari zaidi zikipatikana.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...