Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo ofisini kwake wakati akielezea alivyoshambuliwa na kudhalilishwa na viongozi na wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika eneo la Isakamaliwa,Mjini Igunga juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario alionyesha picha zilizochapishwa kwenye magazeti kadhaa zilizokuwa zikionyesha kile kilichompata kutoka kwa viongozi na wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario akiendelea kuongea na waandishi wa habari waliofika ofisini kwake leo kusikiliza mazungumzo yake.
Hati ya Polisi ya vipimo vya hospitali aliyopewa Mkuu huyo wa wilaya ya Igunga baada ya kushambuliwa na viongozi na wafuasi wa CHADEMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. CHADEMA sasa ni janga la kitaifa. Tusipokiangalia hiki chama kitatupeleka kwenye vita. Kila kitu wao ni mabavu na udikteta tu. Jamani tunaelekea wapi?

    ReplyDelete
  2. Hii nchi inakwenda pabaya maaana vyama vya siasa vinafikiri tayari vimeshakuwa serikali. Sasa ikiwa kila chama cha siasa kitakuwa na sheria yake mambo yatakwendaje?

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli CHADEMA wanawadhihirishia watu kuwa sio wanasiasa wa kweli bali ni watu wanaofanya vitendo vya aibu na kufuru. Wanapaswa wajue kuwa kitendo cha kumvua huyu mama hijaab ni kitendo cha kuudhalilisha Uislamu ambao ndio uliomfanya yeye ajifunike kichwa. Kwa kweli CHADEMA wanatakiwa wawaombe radhi Waislamu na wamuombe radhi huyu mama. Huu kabisa sio ustaarabu wa kitanzania

    ReplyDelete
  4. TUKISEMA CHEDEMA HAWANA MAANA TUNAONEKANA WATU WA CCM INAKUWAJE MKUU WA WILAYA KTK WILAYA AMBAYO YEYE NDIE RAIS ANAYETAWALA PALE HAO WANASIASA WA UCHWARA WA CHADEMA WAKAMPIGE NA KUMFANYIA FUJO HALAFU NDIO MWATAKA TUWAKABIDHI NCHI YA TANZANIA MUIONGOZO NYIE?HAIWEZEKANI HATA KIDOGO YAANI HAMFAI HAMFA HAMFAI HATA KIDOGO TUNAWACHOKA SASA TUNAOMBA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE NA WAADHIBIWE KWA KOSA KUBWA LA KUIFANYIA FUJO SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI UWE MFANO KWA VYAMA VYOTE - Mdau wa ughaibuni

    ReplyDelete
  5. Wapendwa tuangalie pande zote mbili. MAMA ALIYEVULIWA HIJABU. Je walimvamia tu na kufanya hivyo? CCM Mara nyingi wameweka viashiria vyakuanzisha ugomvi ili mradi tu wapaete pakushika. Serikali iwe makini sana katika matukio haya. UKWELI UPO KWA MTU MMOJA TU MUNGU. HIVI tutawekeana majanga mpaka lini? Mara wameua, mara wamemwagia mtu tindi kali mara wamevuwa hijabu. KUWENI WENYE MIYO SAFI. HAKUNA KITU KIZURI KAMA KUFANYA AU KUTENDA HAKI. MUNGU ATWAPA HAKI TU HAT KAMA ITACHUKUA MIAKA MINGI. KWANI HATA MOSE HAKUWAVUSHA WALE WA MIISRI KWA URAHISI ILICHUKUA MUDA KWA KIBALI CHA MUNGU.

    ReplyDelete
  6. Maoni ya Anon wa Sat Sep 17.05:04:00 PM 2011,Sat Sep 17.05:25:00 PM 2011,Sat Sep 17.06:36:00 PM 2011,Sat Sep 17.07:02:00 PM 2011. Ni ya mtu mmoja anayejaribu kueneza propaganda. Baada ya kukaa na kushauriwa uongo wa kuongea wamekuja na stori hizi. Huyu mama kama angekuwa amepigwa kweli asingesema ataenda kwenye mkutano wa Dr. Slaa, halafu mbona imechukua muda hivi mpaka kuja na stori hii baada ya kuwafungulia kesi wabunge wa CDM wanaopiga Kampeni za nguvu dhidi ya CCM. Hii inazidi kuporomosha umaarufu wa serikali na vyombo vyake katika kusimamia haki.
    1. Yaani wanatumia mpaka Hospitali, Polisi na watatumia mahakama ili kukandamiza wana CDM

    2. Serikali kama ingekuwa makini ingesimamia haki, kuchukua hatua kwa upendeleo ni kuondoa imani ya wananchi kwa vyombo hivyo. Ninaamini CDM wana mkanda wa video ya tukio zima na watautoa mahakamani kuonesha dhulma hii. Hebu tuheshimuni sheria jamani, Kwa nini tusiache wananchi wa IGUNGA waamue wanayetaka kuwa mbunge wao kwa nyia ya kura halali?.

    ReplyDelete
  7. sisi kama watanzania tunahaja ya kuzingatia utawala bora kwa kuheshimu viongozi wetu na maamuzi wanayotoa na kama kunahaja ya kuhoji mambo ya kimsingi tufate taratibu za kisheria na sio kumkwida mkuu wa wilaya .tabia hii imeota mizizi matukio ni mengi sana ya uzalilishaji wa viongozi wetu tunaomba sheria ichukue mkondo wake hii ndio changamoto kubwa kwenye kazi za kiutawala na za kusimamia sheria

    ReplyDelete
  8. Itakuwaje Mkuu wa wilaya anashambuliwa, polisi walikuwa wapi? Hiyo kasheshe, au alijiendea peke yake?

    ReplyDelete
  9. Watanzania tusikurupuke tu na kutoa lawama kwa chadema. CCM inatafuta ushindi wa mezani. Kwa hiyo wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanaichafua chadema kwa jamii. Si ajabu ndio haohao waliomwagia mtu tindikali ili ionekane ni chadema. Lakini kama mdau mmoja alivyosema, mwisho wa fitna utafika. Mkumbuke kuna Mungu anayeujua ukweli na atampa haki yule aliyesimamia ukweli.

    ReplyDelete
  10. Sheria zinasema wazi kuwa wakati wa kipindi cha kampeni hairuhusiwi kiongozi yoyote wa serikali kufanya mikutano au vikao katika sehemu ambayo kampeni na uchaguzi utafanyikia. Sasa huyu mama ilikuwaje akaenda kufanya kikao mita 400 tokea zilipokuwa zinafanyika kampeni za Chadema? Mbona huu uvunjwaji wa sheria hazungumzwi? Au ndio kuonyesha kuwa viongozi wetu wako juu ya sheria?

    ReplyDelete
  11. sipendi siasa ila CHADEMA siipendi kabisaaa! kama wamedata vile!

    ReplyDelete
  12. Kwa aina hii ya vijana wanaotoa maoni haya tusitegemee mabadiliko TZ, wa2 hawana reasoning capacity kabisaa wanakurupuka tu na kucomment kwenye mambo ambayo hawajayafanyia utafiti kabisa, its better to remain silent rather than commenting nosense.

    ReplyDelete
  13. Mtaichukia CHADEMA bure tu lakini mtambue hao ndio wanajitahidi kuinyoosha hii nchi. Bila ya kuweka bayana mambo kama haya ya viongozi kukiuka taratibu zilizowekwa mjue nchi itakuwa haiendi hii. Ni lazima tuwekane sawa.

    Kumbukeni CHADEMA ndio wamefanya mpaka sasa angalau viongozi wanakuwa makini kwenye maamuzi ya nchi hii na wanafikiri kwamba siku yakifahamika haya itakuwaje?

    na ndio wanafanya angalau sasa tunaelekea kwenye uwajibikaji wa kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...