MFANYABIASHARA na mwanamichezo maarufu nchini, Azim Dewji amesema kuwa, kamwe haafikiani na utetezi unaotolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetileh Osiah anayedai Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen (pichani kushoto) hawezi kufukuzwa kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili.
Dewji aliyewahi kuifadhili Simba na kuipa mafanikio makubwa Afrika, alisema jijini Dar es Salaam kuwa, wadau wana nafasi kubwa katika ustawi wa soka ya Tanzania, hivyo wasipuuzwe kwa majibu ya juu juu.
Alisema: “Nimesoma taarifa inayomnukuu Katibu Mkuu wa TFF kwamba Paulsen hawezi kutimuliwa kwa sababu ana mkataba wa miaka miwili, tena kwa sababu ya maoni ya wadau.
“Binafsi nasema hii si sahihi. Kocha anapimwa kwa vigezo vingi, lakini kama ameshindwa kazi na haoneshi dalili za kuelekea kufanikiwa, kwanini aendelee kuachwa kazini? Nahisi Angetile amepotoka na kamwe siafiki utetezi wake.”
Dewji aliongeza kuwa, kocha huyo raia wa Denmark alipaswa kuifanyia mapinduzi ya soka Stars, lakini anashangazwa kuona kila kukicha akifanya sawa na waliomtangulia, kuita kikosi kwa ajili ya mechi fulani huku akiwatumia wachezaji `wazee’ badala ya kuibua na kulea vipaji vipya kwa ustawi wa soka katika miaka ijayo.
![]() |
Dewji (kulia) akiwa na mbunge wa Sumve Mh Richard Ndassa na Waziri Naibu Waziri wa Nishati na madini Mh Adam Malima siku Uwanja mpya wa Taifa ulipofunguliwa |
Osiah, jana alikaririwa na vyombo vya habari akimtetea Poulsen baada ya wadau mbalimbali wa michezo nchini kuhoji uhalali wa kocha huyo kuendelea kutafuta fedha za Watanzania, ilhali haonyeshi mwelekeo wowote, zaidi ya kuporomosha kiwango cha wachezaji wa Taifa Stars.
Miongoni mwa wadau hao ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu aliyeonesha hofu ya Tanzania kutonufaika na lolote kutoka kwa kocha Poulsen.
Akizungumza na waandishi wa habari za michezo juzi, Osiah alisema: “Tunaheshimu maoni ya wadau wetu, akiwamo Mbunge Mangungu (Murtaza), ila lazima tuelewe kuwa Poulsen yupo kisheria na mkataba wake ni wa miaka miwili, hivyo hatuwezi kumuacha kwa mtindo wanaoutaka wao.
Poulsen aliyetua nchini kuirithi mikoba ya Mbrazil Marcio Maximo mwaka 2010, hajapata mafanikio makubwa akiwa na kikosi cha Stars, ukiondoa `ngekewa’ ya kutwaa Kombe la Challenge, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994. Ilishindwa kwa `matuta’ kuanzia hatua ya makundi hadi fainali.
Na hata baada ya kuingia katika michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2012 na ile ya Kombe la Dunia mwaka 2014, Stars imeendelea kuwa ile ile ya kubahatisha uwanjani, hali inayompa wakati mgumu Poulsen aliyewabwaga wenzake watano katika mchujo wa mwisho wa kundi la makocha 59 waliokuwa wameomba kumrithi Maximo.
Habari za siku.
ReplyDeleteKama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).
Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
http://blogutanzania.blogspot.com/
kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
Ahsante
Luiham Ringo.
HAYA HII SASA NI HADITHI YA KUCHAMBA KWINGI.......... ALIKUWA MASSIMO AKAFANYA KAZI VIZURI YAKAANZA MANENO NA WASHIKA DAU HAO HAO OH HUYU HAFAI MARA LILE AKAJIRUDIA BRAZILI AMELETWA HUYU SASA YAMEANZA TENA, WADAU HAO HAO WAMEANZA TENA OH HUYU HAFAI WATANZANIA SOKA LETU LITAKUWA KWERI KWA HILA HIZO? Mdau wa ughaibuni
ReplyDeleteMimi nafautiana na hao wadau wanaosema huyu kocha hafai. Mimi namkubali sana huyu kocha. Uteuzi wake unaangalia uwezo wa wachezaji waliopo, huwezi ukamlinganisha Poulsen na Maximo. Maximo katika uteuzi wake alikuwa anaangalia vipaji vya vijana na si kuendeleza uwezo wa wachezaji waliopo, hivyo ingefaa Maximo afundishe timu za vijana na sio timu ya wakubwa. katika soka kuna kuibua vipaji vya vijana na kuendeleza vile vya wale wazamani ambao wanaunda timu ya timu ya taifa wakati huohuo vijana wanapanda polepole, Poulsen ameliweza hilo wakati Maximo alishindwa kwani katika miaka 4 ya maximo hakuwa na timu ya taifa ya kudumu Poulseni ameweza kuwa na timu ya kudumu kwa muda mfupi tuu, kila kukicha Maximo alikuwa anakuja na timu mpya ndio maana hakufanikiwa. Ukilinganisha uwezo wa timu ya taifa wakati wa Poulsen ni mkubwa timu imenyakua kombe la Challenge na bado ina nafasi ya kuingia fainali za kombe la Afrika Equatorial Guinea kama itaishinda Morocco haya ni mafanikio ya Poulsen Maximo hakuweza. Hii timu imezitoa jasho Algeria na hata hiyo Morocco yaweza fungwa kwao kama hatutamkatisha tamaa kocha na wachezaji.Timu yetu ina level nzuri huwezi ilinganisha na vibonde Comoro, Mauritius, Somalia n.k. Tatizo lilipo ni kwamba timu yetu haipewi mechi za kimataifa za majaribio na timu kalikali, hii ingesaidia.
ReplyDeleteKwa kweli inachekesha sana, sasa na huyu amekuwa hafai na ni wadau hao hao waliokuwa wakimponda Maximo. Siku zote huwa nasema kwamba Tanzania tatizo si kocha. Naamini hata akija kocha bora duniani kwa sasa, ama wale wote tunao waamini kuwa ni bora mno yatakuwa yaleyale. Tatizo letu kubwa ni kwamba tunawachezaji wenye viwango vidogo sana. Hii inasababisha kutofanya yale tunayo tarajia katika mashindano makubwa. Nakubali kocha anasehebu kubwa kunufaisha timu ila filosofia yangu ya mpira ni kwamba wachezaji kwanza alafu kocha ndo anafuata. Ukitaka kujua kama tunawachezaji wenye viwango vidogo jaribu kuangalia klabu zetu zinafika wapi katika mashindano ya kimataifa. Siku zote tunawaonea hao washelisheli, timu kutoka Botwsana, Angola, Malawi, Zambia na n.k na marazote tukijitahidi sana ni kufika raundi ya pili ama ya tatu kwenye hatua ya mtuano, hata makundi hatufiki. Kocha si suluhisho kupeleka soka la Tanzania mbele. Suluhisho ni kuwa na mikakati kabambe ya kuibua vipaji vya watoto na kuwafundisha mpira wa kisayansi mapema. Hii itasaidia kutoa wachezaji kucheza ligi kubwa duniani. Timu zote kubwa Africa, Nigeria, Cameroon, Senegal, Ivory Coast na nyinginezo hutegemea wachezaji wanaocheza ulaya kwa karibu alilimia themanini na ndo maana ubora wao unaonekana. Sisi tunategemea wachezaji toka Yanga, Simba, Azam, Mtibwa na kwingineko, ambapo hata wao wanategemea wachezaji wa kigeni katika timu zao. Wadau tunapiga sana kelele pila kufanya suluhisho sahihi la tatizo. Kama mnadhani makocha ndo watapandisha kiwango cha soka hapa Tanzania, bila kuangalia mzizi wa tatizo tutafukuza sana makocha. Tujipange tuwe na wachezaji bora na wenye viwango vya kimataifa.
ReplyDeleteLigongo
Watanzania wengine ni watu wa ajabu. Kila kocha mnalalamika tu. Massimo kelele nyingi. Poulsen kelele nyingi. Sasa nyie mnataka nini? Huyu Poulsen kaja kawapa kombe la chalenji. Halafu Taifa stars ipo kwenye kundi gumu sana ukizingatia Morocco, Algeria na Central Africa si Mauritius, Rwanda au Burundi. Hata Ivory coast ukiwaweka kundi moja na Morocco na Algeria watakaa chini na kutafakari waanze wapi. Hili hatulielewi! Alipoifikisha stars kwenye kundi ni mahali pazuri. Ana pointi tano na bado ana matumaini ya kufuzu. Sasa mnataka nini? Wakati huu ilibidi mumpe ushirikiano. Maneno maneno hayafai kwani Simba na Yanga hufanya nini zikicheza na timu za Morocco au Algeria. Jibu ni zinatunguliwa. Angalia kwa Wydad simba ililala 3-0. Sasa acheni kuwa watu msioelewa. Huyu kocha mzuri. Mechi waliyoufungwa Central Africa kila mtu anajua bao la stars lilikataliwa. Sasa yeye afanye nini? Nadhani Poulsen ni kocha mzuri. Tanzania si Ivory Coast au Nigeria kisoka. Hivyo ujuaji mwingi haufai!
ReplyDeleteNakubaliana na Azim. Hata kama Poulsen ana mkataba wa miaka mia haimaanishi kuwa hauwezi kuvunjwa. Pande mbili zinapoingia mkataba inapaswa kuwepo kipengele cha kuvunja mkataba huo ambacho kitaainisha masharti yake. Mkataba huu kati ya Poulsen na TFF utakuwa na wa ajabu sana kama utakuwa hauna kipengele kama hiki. Kama kipo, basi mkataba unaweza kuvunjwa ili mradi masharti yatimizwe.
ReplyDeletesa mkataba wa Poulsen uvunjwe kwa misingi gani? Kocha naposhindwa kazi mkataba ndipo unapovunjwa. Poulsen hajashindwa kazi. Timu inacheza na mpaka sasa timu inaheshimika. Waambie Wamoroko au Wanigeria kesho unacheza na Taifa Stars watajiandaa. Taifa stars si tena mteremko. Wacheni kumchafulia jina Poulsen. Hivi mnafikiri mkimfukuza atakosa timu ya kufundisha? Angalieni Kocha Micho. Yanga soka bofu. Mkamfukuza sasa anatamba na Al Hilal. Ameifanya Al Hilal moja ya timu bora Afrika. Sasa kwani alishindwa yanga au timu ya yanga ndiyo iliyoshindwa. Mimi kama Mtz namtakia mafanikio Poulsen. Namwona akaze moyo hata kama watz hatuna shukrani, ainoe timu ili tuifunge Morocco. Poulsen watanzania kamamimi tupo na wewe na tunakupenda kama kocha. Usiwasikilze kina Dewji. Ziba masikio na andaa timu kwa mechi ya Morocco. Congratulations Poulsen! Poulsen, we love you!
ReplyDelete