Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, imedaiwa kuwa hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi, ya ama kulipa faini au kwenda jela kwa kitendo cha kuidharau amri halali ya mahakama, bado haijasitishwa.

Hivi karibuni, Jaji Nchimbi wa Mahakama ya Ardhi alitoa hukumu dhidi ya Rutabanzibwa ama kulipa faini ya sh. 500,000 katika kipindi cha siku tano, au kutumikia adhabu ya miezi sita kwenye gereza la Ukonga, endapo atashindwa kulipa faini hiyo, kwa kitendo cha kuidharau amri halali ya mahakama hiyo.

Mbali na hukumu hiyo, Jaji Nchimbi pia aliwahukumu Kaimu Kamishna wa Ardhi, Bramsden Sichone na Mkurugenzi Mipango Miji, Albina Bura, kutumikia adhabu hiyo kutokana na kutenda kosa hilo la kudharau amri halali ya mahakama hiyo.

Hata hivyo, mwishoni mwa wiki hii iliripotiwa kuwa amri ya kutaka Rutabanzibwa na wenzake walipe faini au kutumikia kifungo, imesitishwa kwa muda kusubiri uamuzi wa ngazi ya juu baada ya jalada ya kesi hiyo Namba 14 ya 2009, kupelekwa kwa Jaji Mkuu, Othman Chande, baada ya Rutabanzibwa na wenzake kuomba isitekelezwe kwanza hadi jalada hilo litakapopitiwa upya na mahakama ya juu.

Jaji Othman aliita faili hilo ili kujiridhisha na uamuzi uliofanywa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ambao ulilalamikiwa na Wizara ya Ardhi

Akizungumza Dar es Salaam jana, mmoja wa mawakili wanaotetea wadai wa kesi hiyo ambaye hakupendwa kutajwa jina lake, alidai amri ya mahakama haijasitishwa licha ya faili la kesi hiyo kuitishwa Mahakama ya Rufaa.

"Rutabanzibwa na wenzake bado wanatakiwa kutekeleza hukumu... ni kweli faili lao liko Mahakama ya Rufaa, lakini hakuna mahakama iliyotengua amri ya hukumu... Mahakama ya Rufaa kuitisha faili si kutengua amri ya mahakama ya chini.

"Ili hukumu kama hiyo itenguliwe inatakiwa kukutanisha jopo la majaji watatu, hilo halijafanyika, ndiyo maana Rutabanzibwa amelipa faini, ingawa bado hajasaini hati ya viwanja alivyoagizwa... kwa maana hiyo hajatekeleza agizo la mahakama.

"Kwa kigezo hicho, Rutabanzibwa na wenzake wanatakiwa kuwa gerezani... sasa hivi tunasubiri nakala ya hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ili tumpe Kamanda Suleiman Kova akawakamate na kuwapeleka gerezani.

"Isitoshe mpaka sasa Rutabanzibwa na wenzake hawatakiwi kuendelea kukaa ofisini na kufanya kazi kutokana na kushtakiwa kwa makosa ya jinai... wanatakiwa wawe gerezani," alidai wakili huyo.

Wakili huyo aliyebobea alisisitiza kuwa kisheria, Rutabanzibwa na wenzake wamepoteza haki zao zote za mafao kazini na hawatatakiwa kuendelea kuwepo ofisini, labda wakate rufani na kushinda.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kuhusu kashfa iliyoikumba wizara yake, alisema hana taarifa kuwa hiyo ni kashfa kwa vile suala bado liko mahakamani na halijapatiwa ufumbuzi.

"Wizara yangu haina kashfa na Katibu wangu hana kashfa, kesi iko mahakamani, tusubiri uamuzi utoke kwanza," alisema Prof. Tibaijuka.

Ilidaiwa kuwa Rutabanzibwa alikataa kusaini hati ya viwanja No. 1272 na 1273 vilivyopo Msasani Peninsula, ikiwa ni makubaliano yaliyofikiwa baina za Kampuni ya Oysterbay Properties Ltd, Kahama Minning Corporation Limited, Mahakama, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna wa Ardhi.

Rutabanzibwa alikataa kusaini hati hizo akidai kuwa uamuzi huo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ni uzembe na ukaidi kwa Wizara ya Ardhi.

Jaji Nchimbi alibainisha kuwa amri ilitolewa na mahakama hiyo kutokana na muafaka uliofikiwa baina ya kampuni za Oysterbay Properties Ltd, Kahama Minning Corporation Ltd, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Kamishna wa Ardhi kuhusiana na viwanja No 1272 na 1273 vilivyoko Msasani Peninsula, Dar es Salaam.

"Makubaliano yaliyofikiwa na pande zote mbili yaliifanya mahakama hiyo itoe tuzo kwa wadai kukamilishiwa viwanja hivyo na wadaiwa wote kwa pamoja," alidokeza na kuongeza tuzo hiyo ilikuwa ni amri halali kwa wadaiwa kuitekeleza bila ubishi wowote.

Jaji Nchimbi alisisitiza ni wajibu wa vigogo hao wa wizara hiyo kutii amri hiyo kwa kuwapatia hatimiliki ya viwanja hivyo wadai hao wawili, na pia waliagizwa kutoa hatimiliki hizo ndani ya siku tano.

Pia aliagiza vigogo hao wa Wizara ya Ardhi wawe wamesaini hatimiliki ya viwanja hivyo na kuwapatia wadai hati hiyo ndani ya siku tano, kitu ambacho hawajakitekeleza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mwisho wa Ubaya aibu,na ndio kitakachomkuta Bwana Rutabanzibwa,alipokuwa katibu Mkuu Mambo ya ndani alikalia vyeo vya watu mpaka alipoondoka ndio wakapandishwa sasa jela inanukia.

    ReplyDelete
  2. Mimi nakubaliana na wewe unapohukumiwa kwenda jela hauwezi kusema nasubiri rifaa kwanza,unatumikia kwanza adhabu yako mpaka rufaa yako inapoamuliwa ndio inauwezo wa kutengua hukumu a mifano tunayo Mingi,sasa hawa Jamaa ni kwamba hawalijui au walitaka kuupotosha uma walipotangaza kutenguliwa kwa hukumu dhidi yao? Hata ofisini hawatakiwi kuwepo tena wasubiri hilo jopo la hao majaji watatu wakae na kuibariki au kuitengua.

    ReplyDelete
  3. Maajabu na ndo maana tulisema mbowe kukamatwa ilikuwa uonevu, mbona yeye huyu alikuwa waziri hakamatwi ila aliye mbunge alikamatwa? Serikali angalieni vema maamuzi yenu, tunawaangalia na kutegemea human right it may work over there. Please michuzi usinibania hata kama nimechafua hali ya hewa nivumilie tafadhali

    ReplyDelete
  4. story ya kukalia vyeo vya watu ndio zao nshomile same was for my dad till wen the nshomile alipostaafu then my dad akapandishwa cheo hawa watu ni wakabila sana.

    ReplyDelete
  5. Mbona comments nyingi za kipuuzi humu. Mara sijui baba yangu alinyimwa cheo na nshomile--who cares! what does that have to do with this story- labda baba yako vitu havipandi--tehe tehe!!! (i am joking of course, but i presume you'll get my point). Wise people once said, "what you say is a reflection of self." Acheni kutukana na kukashifu asilia ya mtu, it makes you look small-minded and petty, and even worse, ignorant. Michuzi usiibane hii comment kwa sababu huu ushenzi upo mwingi sana kwenye blog yako.

    Anyway, endelea kutuletea story zaidi kuhusu hii case.

    ReplyDelete
  6. Nimefurahia comment iliyowaponda kina Ishomire kuwa ni wakabila. Kilichonifurahisha sio ujumbe katika hiyo comment, bali ni jinsi gani Michuzi alivyokuwa muungwana akaamua kuiweka hadharani wakati yeye mwenyewe ni Ishomire. Keep it up michuzi. Watu tusipokubali kuambiwa ukweli hatutabadilika. Hata mimi nilishafanya kazi na hii jamii sehemu mbalimbali. Kwakweli hawakunitendea haki hadi nikaamua kutafuta kazi sehemu nyingine.

    ReplyDelete
  7. Kina Ruta jamani msaidini Rais, nchi hii in matatizo mengi Mkuu wa nchi anataka watu wanaomsaidia, sio kutia wananchi hasira.

    ReplyDelete
  8. Maoni mengine bwana...Hawa nshomile watu huwa hawawaelewi...nshomile tabia zao kama wahindi. Kama hategemie faida kutoka kwako hakusaidii ng'o! Mie baba si nshomile, lakini ana rafiki yake nshomile kwenye wizara fulani ametusaidia sana....hawa watu huwa ni wazuri kwa sabb mara zote hutaka sifa. HUWA HAWATAKI KUONEKANA WAMESHINDWA KAZI.bRAVOOOOOOOOOOOOOONSHOMILE JUUUUUUUUUUU!

    ReplyDelete
  9. Hawa wako wengi wenye kubania maendeleo ya wengi lakini hawajui ukibania mtu hiki huwa pengine ni heri yake anakuja kupata kizuri zaidi. Ile ofisi ya scholarship pale wizara ya elimu ya juu kuna yule mama Ubaya na Abdalla Abeid bom sana watu hawa, washakoshesha watu wengi nafasi zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...