Mchezaji wa timu ya mchezo wa vishale (Darts) ya Safari Darts Club ya Jijini Mwanza,Prosper John akirusha moja ya vishale vyake wakati wa mechi yake dhidi ya Mchezaji Hatim Lamuwala (hayupo pichani) katika mchezo uliochezwa jioni hii katika ukumbi wa Redoch Hall,Jijini Tanga ikiwa ni mwamzo wa mashindano ya mchezo huo wa vishale ya Taifa ambayo yanakutanisha timu za kutoka mikoa 16 ya Tanzania Bara yaliyodhaminiwa na Kampuni ya bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Safari Lager.
Mchezaji wa timu ya mchezo wa vishale ya Magereza Kilimanjaro,Ramadhan Simba akijiandaa kurusha moja ya vishale katika ubao maalum wa kuchezea mchezo huo jioni hii katika ukumbi wa Redoch hall jijini Tanga.Mashindano haya ya "Safari Lager Tanzania Darts Championship" yamefunguliwa rasmi leo jijini Tanga na kuhudhuliwa na timu za kutoka mikoa 16 ya Tanzania bara.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...