
Kwa bidii zangu zote ninawatafutia soko la nje Wanamiziki wote wa Tanzania ili kazi zao zikubalike kazi zao kuuzika katika soko la nje ya Tanzania kupitia kampuni yangu ya ”Music Studio Of Learning – MSOL”.
Nataka kujenga Studio ya mziki (MSOL) kwa ajili ya kurekodi, mastering na kutengeneza albamu zao nje ya Tanzania katika kiwango cha kimataifa na kuzisambaza ndani na nje ya Tanzania, na kwa kutoa elimu ya kurekodi kwa kutumia digitali na kufundisha sheria za miziki ya Tanzania na duniani kote na hasa kuhusiana na jinsi ya kuandika mikataba katika kazi zao. Elimu zote zitatolewa na Waalimu kutoka Sweden kwa gharama za MSOL kwa usimamizi wangu mwenyewe.
Kutoa elimu ya kibiashara za miziki kwa Wanamiziki wote wa Tanzania nchini. Elimu hiyo pia itatolewa na watalaamu kutoka Sweden kwa gharama za MSOL chini yangu.
Natanguliza shukrani zangu kwa Balozi wetu wa Tanzania nchini Sweden (Stockholm) kwa maelekezo yake mazuri sana , pia nawashukuru viongozi wa BASATA (Dar es salaam) kwa kunipokea vizuri barua yangu na simu niliyoongea nao LIVE, ila bado sijapata maelekezo ya kutosha kitu cha kunifanya ili niendelee mbele na shughuli yangu hii.
Kutokana na kubaki njia panda hii, naomba mawazo yenu wadau wengine mnisaidie nifanye nini ili nielewe ninapokwama ni wapi na kwanini, na nifanye nini kuwatengenezea mazuri zaidi Wanamiziki wetu wote wa Tanzania Bongoflava na wengine wote hadi miziki ya zamani? Mimi ninaelewa ninachokitaka. Mbona ninaambiwa kuwa Tanzania eti kuna ”Mafia?, ni kweli? na kwanini?”.
Hadi sasa hivi hakuna aliyeniambia kitu kibaya katika ushauri wao (kwa maoni yao), ila watu wote naona wamejitahidi kunipa picha kamili ya Tanzania ili nielewe ninakodhamiria kwenda kufanya shughuli zangu kuwa kuna nini!. Sidhani kama nitakuwa ni adui wa biashara hiyo kwa yeyote Tanzania. Kwa sababu na nia yangu nasema wazi kuwa sizuii nia nzuri ya mtu kuiendeleza miziki ya Tanzania na wanamiziki wa Tanzania na biashara zao zote za miziki zimhusuzo mtu yeyote badala yake naomba tushirikiane kwa nia ya kuwaendeleza Wanamiziki wa Tanzania.
Nawaomba pia wadau mnipe maoni yenu na hasa Wasanii, Wanamiziki wanieleze wanachokitaka mimi niwafanyie nini? Mimi siji Tanzania kushindana na mtu katika shughuli za biashara bali ni kutoa msaada kwa Wanamiziki na yeyote aliye tayari kushirikiana na mimi kwa shughuli hiyo nipo tayari kushirikiana, nawaomba tuwasiliane.
Peters Mhoja, Gävle-Sweden
+46 70 511 47 69 begin_of_the_skype_highlighting +46 70 511 47 69 end_of_the_skype_highlighting
Mdau mjasiriamali hongera kwa kuwa na mawazo ya kuendeleza TZ. Lakini mdau TZ soko lake la muziki ni dogo sana maana watu wengi hawana utamaduni wa kununua miziki ukilinganisha na watu wa Sweden au nchi nyengine za Ughaibuni. Pia Mdau muziki wa TZ ni ngumu kupata soko la ng'ambo kutokana na lugha. Inawezekana umeona muziki wa waafrika unauzwa ghali huko ughaibuni, lakini cd ngapi zinanunulia? Wanamuziki wengi wa TZ wakija ughaibuni wanaishia kupiga muziki kwenye bar za wabongo au kwenye festival za manispaa ya vitongoji ambazo hakuna viingilio. Ningekushauri ufanye utafiti wa kutosha maana hiyo pesa yako ya pensheni unaweza ukaimaliza bure bila ya kuurejesha hata shilingi!!
ReplyDeleteungeweka e mail basi mheshimiwa sidhani kama wadau wa tanzania watakupigia simu!
ReplyDeletekuhusu ushauri fani ya burudani tanzania iko nyuma sana ndio maana hakuna mwanamziki yoyote mwenye nyumba ya maana, akiba ya kutosha benki na mwenye uhakika wa kukidhi mahitaji ya watoto wake inavyotakiwa.
kwa hiyo kuendi kushindana, unaenda kushirikiana na wadau walioko sababu fani ni changa. Wao wanaofikiri unashindana wana mawazo mafupi.
Hongera sana Mr. Mhoja kwa wazo lako zuri la kutaka kuinua maendeleo ya muziki nchini , lakini kabla hujafanya yote ningeomba uangalie swala la COPY-RIGHTS,, katika uchunguzi wangu ndani na nje ya Tanzania, nimekuwa nikisikia miziki mingi tu 'ya nyumbani ikipigwa kwenye maparty ,Radio hata clubs kubwa..Lakini hakuna hata mmoja aliyekwishaniambia amenunua CD ya mmoja wa wasanii..zaidi ya kudublicate... toka kwa mtu mwingine? je kampuni yako italidhibiti vipi swala hilo ..
ReplyDeleteBIG IDEA! GO FOR IT MDAU ninakuunga mkono kwa asilimia 1000% You gonna make it na utaiteka africa nzima watakuja kurekodi katika studio yako. Kama itatokea utauza share nitakuwa wakwanza kununua!
ReplyDeleteMdau USA
samahani kwa hili nitakalo sema, naomba ukipata muda unipe call kwenye namba hii0786224585, ili nikupe machache kabla hujamaliza suala la kukamilisha hiyo studio, kwa ufupi nimeshafanya hivyo mimi binafsi lakini niliishia njiani, ndio nataka ni share na wewe ugumu uko wapi
ReplyDeleteuunajua mim ni mtanzania naishi hapa california.Nimewaza sana hili jambo,na pia nimeshangaa kuona kwamba kuna mtu tulikuwa tunafikira the same.
ReplyDeleteMimi nilkuwa nataka kufungua entertaiment company,ambayo itatengeneza video,na music recording.
Tatizo langu mimi sina uzowefu wala sijasomea sound engineering au music production.
Lengo langu ni kusaidia vijana chipukizi ambao hawapti sauti na kutoka,pia kuboresha kazi za wasanii,kuinua tamaduni zetu hasa katika ngoma za asilia,na documentary kuhusu nchi yetu nk.
najua its a big dream,hela sio tatizo sana.bali ni jinsi ya kustructure the idea and build an empire.
mimi ushauri wangu,usisubiri kuambiwa tho maoni ni mazuri sana,ila fanya kile roho yako inakutuma.
Mungu akuonyeshe njia mzee.
KIDO