Alhaj Abubakar Msalali Kibodya amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi.

Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia zilizotufikia sasa hivi, Msiba uko mtaa wa Nyang'oro, Upanga, jijini Dar es salaam jirani na msikiti wa Maamur.

Taarifa hizo zimeongezea kusema kwamba maziko yamepangwa kufanyika kesho Jumamosi katika makaburi ya Kisutu baada ya Salat l' Asril

Mola aiweke Roho ya Marehemu Alhaj Abubakar Msalali Kibodya mahala pema peponi

AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mungu amlaze mahali peponi mzee Kibodya. Poleni wote ukoo wa mzee Kibodya,na napenda kumtaja mdogo wangu Yahaya Kibodya(pole sana). Mie Kaka yako Kocha ingawa niko mbali kimwili, daima tuko pamoja.

    ReplyDelete
  2. nikusahihishe mwandishi
    mzee kibodya maefariki mchana milango aya saa sita mchana muhimbili ijumaa ya tarehe 9 sept 2011

    familia ya mzee mahdi na mzee ahmed ajmy wa upanga wanatoa pole zao za dhati kwa familiya ya kibodya khaswa zainab kibodya othman kibodya na ndugu yangu wa karibu yahya kibodya allah ampe malazi mema peponi
    mimi ndogu yako
    saleh mahdi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...