Alhaj Abubakar Msalali Kibodya amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi.
Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia zilizotufikia sasa hivi, Msiba uko mtaa wa Nyang'oro, Upanga, jijini Dar es salaam jirani na msikiti wa Maamur.
Taarifa hizo zimeongezea kusema kwamba maziko yamepangwa kufanyika kesho Jumamosi katika makaburi ya Kisutu baada ya Salat l' Asril
Mola aiweke Roho ya Marehemu Alhaj Abubakar Msalali Kibodya mahala pema peponi
AMIN


Mungu amlaze mahali peponi mzee Kibodya. Poleni wote ukoo wa mzee Kibodya,na napenda kumtaja mdogo wangu Yahaya Kibodya(pole sana). Mie Kaka yako Kocha ingawa niko mbali kimwili, daima tuko pamoja.
ReplyDeletenikusahihishe mwandishi
ReplyDeletemzee kibodya maefariki mchana milango aya saa sita mchana muhimbili ijumaa ya tarehe 9 sept 2011
familia ya mzee mahdi na mzee ahmed ajmy wa upanga wanatoa pole zao za dhati kwa familiya ya kibodya khaswa zainab kibodya othman kibodya na ndugu yangu wa karibu yahya kibodya allah ampe malazi mema peponi
mimi ndogu yako
saleh mahdi