Mr and Mrs K. Mziray

Pongezi nyingi ziwafikie Baba na Mama kwa kudumisha upendo wenu, na sisi kama watoto tutajitahidi kuiga mfano wenu. Hapa Mzee Mziray na Mama wakiwa katika moja ya Sherehe ambazo wanahudhuria katika kuweza kujumuika na jamii mbali mbali. 
Mungu awape maisha marefu na yenye Baraka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nawapongeza sana hata mimi! Ndoa siku hizi matatizo matupu. Kuna mawifi, mama wakwe usiseme.Kuolewa kwenye familia zingine ni balaa tupu. Mawifi hujitahidi kuharibu ndoa za kaka zao lakini za kwao wanazipaka mafuta. Na wanaume msipozngalia dada zenu watawendesha mkose eka wanawake wa kuzeeka nao.

    ReplyDelete
  2. kula tano mdau, tena siku hizi mawifi wana njaa kali hawataki kuwaachia kaka zao waendelee na maisha yao. hawajali hata watoto wa kaka zao japo hata kupiga cm kuuliza hawajambo n.k na wamegundua mbinu mpya za mawasiliano za kupitia mtandao basi wanajifanya wanaorganize maswala ya kifamilia huku wakiwaengua wake za kaka zao kana kwamba si wanafamilia na wanahakikisha malengo yao yanatimia bila wake za kaka zao kufahamu. hii ni dhulma na dhambi maana Mwenyezi MUNGU anataka ndoa iheshimiwe na watu wote.

    ReplyDelete
  3. sijaelewa Baba na Mama Mziray wanapewa Pongezi za kitu gani? Je ni kwa kuwa kwenye ndoa muda mrefu? Kama ndio mbona haijatamkwa ni miaka mingapi ya ndoa ili wanaoingia ndoani wapate mfano halisi.

    Kwa muonekano wana zaidi ya miaka 25 ya ndoa, nawapongeza nawashukuru kwa taswira hii. Vijana tuangalie mifano hii na siyo ile ya kina Marc Antony na JLo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...