Kwa ndugu watanzania wenzetu:

Kwa niaba ya Watanzania waishio hapa nchini Malaysia nachukua fursa hii kuto salamu za rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali ya meli MV Spice Islander . 

Tumepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za msiba huu. Ingawa tuko mbali na nyumbani lakini tunapenda kuwahakikishia kwamba tuko pamoja katika kuomboleza msiba huu wa kitaifa.

Aidha tunapenda kuwapa pole wale wote waliosalimika na kuokolewa katika ajali hiyo tunamwomba Mwenyezi MUNGU awasaidie mpone haraka ili muweze kuungana na ndugu jamaa na marafiki katika familia zenu.

Tunawapongeza na kuwashukuru wale wote walioonesha moyo wa uzalendo kwa kutoa msaada wa hali na mali katika kufanikisha kuokoa maisha ya watu walionusurika, lakini viulevile hata kuopoa na kuwahifadhi marehemu wetu. Kwa hili tunawashukuru sana na tunamwomba mwenyezi MUNGU awarudishie mara kumi zaidi ya kile mlichotoa.

Tunawapongeza viongozi wa serikali, wanasiasa na asasi zisizo za kiserikali waliotenga muda wao na kuahirisha shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili ili kuungana na ndugu jamaa na marafiki na kwa kuwapa faraja katika kipindi hiki kigumu. Tunawaomba muendeleze moyo huo wa kizalendo.

Mwisho kabisa tunamwomba mwenyezi MUNGU atupe mshikamano na umoja katika kukabili kipindi hichi kigumu cha maombolezo.

Mwenyezi MUNGU azilaze mahali pema PEPONI roho za merehemu wetu . AMINA.

Abel Lyimo
Mdau wa Malaysia
kny. ya watanzania Malaysia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...