BAN KI MOON AOMBELEZA AJALI YA KUZAMA KWA MELI-ZANZIBAR

 Katibu  Mkuu wa  Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemtumia salamu   za rambirambi  Mhe.  Dkt. Jakaya  Mrisho Kikwete,  Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia ajali mbaya ya kuzama kwa kivuko cha MV Spice Islander iliyotokea usiku wa kuamkia septemba 10,2011 na kupoteza maisha ya watu na mali.

Katika salamu zake,Katibu Mkuu amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuzama kwa kivuko hicho katika pwani ya Zanzibar na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja  wananchi wa Tanzania katika kipindi  hiki kigumu

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu na  nakala yake kupatika  Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.  Salamu za pole za Katibu  Mkuu, pia anazituma  kwa Serikali na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar na familia za waathirika wa ajali  hiyo.

 Katibu Mkuu Ban Ki Moon, pia amewatakia kila la kheri na  nafuu ya haraka  majeruhi na  wote walionusurika wa  ajali hiyo.

IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NEW YORK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...