Tanzanian Muslim Community in Washington DC Metropolitan
(TAMCO)
Jumuiya ya Waislam wa Tanzania ya Washington DC Metropolitan (TAMCO) - inajumuika na watanzania wote duniani katika kuomboleza na kuwapa pole wale wote waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali ya meli iliyotokea huko Zanzibar . Pia tunawaombea dua marehemu na majeruhi katika ajali hiyo.
TAMCO inawaomba watanzania wote wanaoishi Maryland , Washington DC , Virginia na states jirani kujumuika kwa pamoja siku ya Jumapili ya tarehe 18/9/2011 kwenye dua ya pamoja kuwaombea marehemu, majeruhi na ndugu waliopoteza jamaa zao.
TAMCO kwa kushirikiana na watanzania wote tutafanya harambee na kukusanya fedha ilikuweza kuzisaidia familia zilizopoteza ndugu pia kusaidia shughuli zote za mazishi kwa wale waliofariki. Tunawaomba watanzania wote kushiriki kwa pamoja kuwafariji ndugu, jamaa na marafiki walioathirika na ajali hii.
Address:
MD 20903
Muda: 5:30 PM - 7:30PM
Uongozi
TAMCO


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...