
WANACCM UK WANAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUOMBOLEZA KWA MAJONZI MAKUBWA AJALI HII ILIYOPOTEZA MAISHA YA WATU TAKRIBAN 200, KUSABABISHA MAJERUHI WASIOJIWEZA NA MSIBA KWA FAMILIA, NDUGU NA TAIFA ZIMA.
AIDHA CCM UK INAWAPONGEZA WATU NA TAASISI MBALI MBALI ZILIZOJITOKEZA KUSAIDIA KUWAOKOA WATU NA KUWAHUDUMIA MAJERUHI NA PIA KUTAFUTA MIILI YA WENZETU WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI.
CCM UK INA IMANI NA SUBIRA KWAMBA SERIKALI ZITAZIAGIZA MAMLAKA MAALUM KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA NA KULETA MAJIBU YA WAZI NA KWELI JUU YA SABABU ZA AJALI HII MBAYA NA KISHA KUCHUKUA HATUA ZA MAKUSUDI ZA UWAJIBIKAJI ILI KUZUIA AJALI ZISIZO ZA LAZIMA ZISITOKEE TENA.
MWENYEZI MUNGU (ALLAH! (S.A.W)…
AWAPOKEE KWA HAKI WALIOTANGULIA KWAKE…
AWAPONYE NA KUWATIA NGUVU MAJERUHI WA AJALI HII…
AWAFARIJI NA KUWAPA AMANI WAFIWA WOTE…
ccm ungeleza. angalau pole yenu ina maakili kidogo kutaka kuwajibisha serikali yenu ifanyike uchunguzi bila mambo kuenda bwelele kama kawaida yao.
ReplyDeletekitonga mrefu