Uongozi wa Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo pamoja na wafanyakazi wake wote unaungana na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wazanzibari wote kutokana na msiba mkubwa uliyoikumba nchi kutokana na kuzama kwa meli ya Spice Islanders tarehe 10/09/2011 wakati ikisafiri kwenda Pemba kutokea Unguja.

Ofisi inatoa pole kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ndugu na jamaa wa wafiwa wote. Aidha, Ofisi inawaombea subira na kupona haraka wale wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Tunamuomba Mwenyezimungu mkarimu azilaze roho za marehemu waliotangulia mbele ya haki mahali pema peponi, Amin.

Inshallah familia zote zilopatwa na msiba huu nazo ziwe na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu.

INNA LILLAH WAINNA ILAIHI RA'AJIUN.
 
Imetolewa na; 
Afisa mawasiliano
Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo
Skina Hamad Salum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...