Amaya ni Beauty Salon & Spa mpya na  ya kisasa kabisa iliyopo katikati ya Jiji la Dar-es-salaam.Ipo nyuma ya jengo la Air Tanzania Corporation(ATC) lililopo katika makutano ya barabara za Ohio Street  na Garden Avenue.Amaya Beauty Salon & Spa inajivunia kuwa Beauty Salon & Spa inayotumia bidhaa halisi(original) kutoka Canada na USA huku ikiwa na wafanyakazi waliobobea katika masuala yote yanayohusu urembo kutokea ndani mpaka nje na wenye ujuzi wa kimataifa.

Miongoni mwa huduma zinazopatikana ndani ya Amaya Beauty Salon & Spa ni pamoja na;
  • Huduma za nywele kwa aina zote za nywele kuanzia kunyoa au kukata style mbalimbali, kusuka,kuweka dawa,ku-steam, kuchana style mbalimbali,kushonea weaving aina zote,kubandika lace wigs,relaxing,kubandika kope,ku-bond nywele,kuweka aina zote za rangi kwenye nywele, kusokota dreads,kutinda nyusi kwa uzi,twisser na wembe, etc
  • Huduma maalumu(specialized treatments) kwa ajili ya mikono na miguu(Manicure and Pedicure) ikiwemo kuosha miguu kwa kutumia mask na paraffin, kuosha mikono,kupaka rangi,kubandika kucha aina zote za rangi mbalimbali/tips,acrylic powder na gel.
  •  
  • Tunafanya facial za aina tofauti tofauti  ikiwemo kutoa chunusi,madoa ya uso nk
  •  
  • Pia tunafanya waxing
  • Tunapamba maharusi,send off,kitchen party na special days kama vile graduation,ubatizo,kipaimara nk
  • Tunauza products mbalimbali kama vile Designers Perfumes kutoka kwa Usher,J-Lo,DKNY etc.Avon Products kama vile Powders,Colognes,body creams,shower gels nk.Make-Up products za Mac kama vile Studio Fix,Powders & Foundations,Eye Shadow,Lipsticks/gloss,perfumes nk
  • Pia tunatoa huduma zote zilizotajwa hapo juu katika vyumba maalumu(Private Rooms) na kwa kutumia products maalumu.

Amaya Beauty Salon & Spa inayo sehemu kubwa ya maegesho ya magari (Parking) yenye ulinzi wa uhakika. Hapo zinapaki limo nane kwa mpigo bila wasiwasi na nafasi inakuwa bado ipo. Ipo wazi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi(6am) mpaka saa moja jioni(7pm) Jumatatu mpaka Jumamosi.

Kwa mawasiliano zaidi tumia simu;  
0716 604495, 
0684 262924 
0753 262 924

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. huko vyumba maalum kuna wahudumu maalum au vipi. unachagua mwenyewe au?. na je inahitaji kuweka order au vipi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...