MAREHEMU DOROTY HUSSEYN CHOMBA
Hatimaye yamepita masaa, siku, wiki na sasa umetimia mwezi mmoja tangu mama yetu mpendwa DOROTY HUSSEYN CHOMBA ulipoitwa kwenye makao yako ya milele. 

Daima upendo wako, ucheshi, sauti yako, ushauri na busara zako zinaendelea kukumbukwa na ndugu na marafiki. 

Unakumbukwa na wanao Jamila, Claus, Kuruthum, Juma na Lulu. Pia unakumbukwa na wadogo zako Luiza, Betty, Salome, Grace, Sophia, Christopher na Angela. 

Tunapenda kuwaalika ndugu, jamaa na marafiki katika misa maalumu itakayofanyika nyumbani kwa marehemu mwenge tarehe 30/09/2011 saa 4:00 Asubuhi. 

Tunatanguliza shukurani zetu kwa watu wote walioshiriki na kutufariji katika kipindi cha chote cha msiba wa mama yetu mpendwa DOROTY .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ohhhh pole mama sote tu njia moja.

    Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.

    Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...