Ujenzi wa Barabara ya Msata kuelekea Bagamoro mkoani Pwani umefika katika hatua nzuri ya kiwango cha lami kama inavyoonekana pichani.Barabara hii ikikamilika itarahisisha sana na kupunguza hadha ya msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro.na hizi ni baadhi ya mashine za kutendenezea barabara hiyo zikiendelea na kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ikikamilika itakuwa poa sana... mtu unakuwa na uhuru wa kuchagua upitie wapi, na mabasi ya kwenda Arusha, Kilimanjaro na Tanga yatakuwa mengine yanapitia Bagamoyo hivyo kuongeza kipato kwa wakazi kando kando ya barabara. Safi sana.

    ReplyDelete
  2. pia itaongeza foleni kuanzia Mwenge mpaka Tegeta....

    Mzozaji

    ReplyDelete
  3. halafu mnasema serikali haijafanya kitu....

    ReplyDelete
  4. Mzozaji, barabara ya mbezi bagamoyo nayo inatengenezwa kwa kuiongeza kwahiyo foleni itadhibitika. Sisi watumiaji wa njia hiyo itatusaidia kupunguza mzunguko..Mzozaji, barabara ya mbezi bagamoyo nayo inatengenezwa kwa kuiongeza kwahiyo foleni itadhibitika. Sisi watumiaji wa njia hiyo itatusaidia kupunguza mzunguko..

    ReplyDelete
  5. Kazi nzuri ila barabara iwe kwenye viwango vinavyo kubalika. Hapo mheshimiwa nampongeza sana, kazi kwa watu wake waitumie ili kuondokana na umasikini.

    ReplyDelete
  6. MWENYE MACHO HAMBIWI TAZAMA KAKA BADO WANA SIASA WAOSHA VINYWA WATAPANDA JUKWAANI NA KUSEMA SERIKARI YETU BURE TU,CHA AJABU SERIKARI HIYOYO NDIO IMEWASOMESHA NA KUFIKIA HAPO WALIPO,BANDARI YA BAGAMOYO IKIKAMILIKA TUTKUWA TUMEPIGA HATUA KUBWA YA MANDELEO YETU.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.WENYE WIVU WAJINYONGE WASHINDWE WALEGEE KWA DAMU YA YESU.

    ReplyDelete
  7. Anoy wa sept 03.05.00 am kama Kikwete kwao kungekuwa Monduli hii barabara isingejengwa. Kama Kikwete kwao kungekuwa Kigamboni ungekuta daraja limeshakamilika.

    ReplyDelete
  8. Anonymous wa 12:42:00 eeeh jamani hamuna shukurani hata kidogo. Kwani Kikwete amejenga barabara moja tu katika miaka yote hii aliyokuwepo madarakani?

    Punguzeni roho mbaya zenu

    ReplyDelete
  9. Anon wa Sep 25 12:42:00: Najuavyo Kikwete ni mtu wa Chalinze. Hivi hiyo barabara ni yakwenda Chalinze?

    ReplyDelete
  10. mie napongeza sana hii, lakini kuna kitu kinanitatiza sana, kila siku serikali sijui inatanua wapi na inawalipa wahusika wa maeneo hayo wakajenge kwengine, sasa huko kwingine hakutokuja kutanuliwa, halafu swala la kuhamisha watu kigamboni sijui kujengwe mji gani, hivi hao jamaa wawekezaji hawajaona sehemu yoyote zaidi ya kigamboni si kuna mapoli kibao hayakaliwi wala nini si wakajenge, kama poli lote la pale kuanzia mlandizi mpaka ruvu ni kubwa zaidi ya kigamboni, kwani sisi masikini hatupaswi kukaa sehemu nzuri mpaka kila siku muwe mnatuhamisha hamisha jamani, mie sitoki kigamboni bhana

    ReplyDelete
  11. Dah mshikaji hapo Geography imekupita kushoto, Wilaya ya Bagamoyo ina miji mingi bana.Msata, Chalinze zote zipo ndani ya wilaya ya Bwagamoyo..! Halafu mheshimiwa yeye yupo kijiji cha msoga.So Hiyo barabara inawarahisishia watu wa chalinze, Msata,Doma, hata Ubena zomozi kufika kwa haraka makao makuu ya wilaya yao ya Bagamoyo.Wanaepuka mzunguko wa kupitia DSM. So mimi naona JK kafanya la maana, mtu kwao bana. Hata kama mm ningekuwa JK ningefanya vitu vya maana home.Ukipata kitumie mshikaji.Mkapa kajenga daraja la Rufiji lakini mwenyewe anapozi Lushoto. Mipango ni kuchagua. Bigup michuzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...