Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wazamiaji 12 kutoka nchini Afrika ya Kusini, wamewasili usiku wa kuamkia leo mjini Zanzibar kuungana na wazamiaji wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini ili kufanya uhakiki wa kujua kama bado kuna mili iliyokwama kwenye Meli ya MV Spice Islander iliyozama chini ya bahari eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa Jumamosi wiki iliyopita.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Aboud Mohammed, amesema kuwa wazamiaji hao wamewasili wakiwa na zana za kisasa za uzamiaji na kwamba kazi ya kwanza itakayofanywa na timu hiyo ni kuhakikisha kuwa wanaifikia meli hiyo iliyozama umbali wa karibu nusu kimometa kwenye mkondo mkubwa wa maji na majabali.
Bado Serikali na wananchi mbalimbali wanadhani kuna miili ya watu waliokwama katika vyumba vya meli hiyo tangu ilipozama usiku wa Jumamosi Septemba 10 mwaka huu ikiwa na idadi ya watu isiyojulikana.
Makundi ya wananchi wamekuwa wakitaja idadi ya ndugu na jamaa waliosafiri na Meli hiyo na ambao hawajapatikana wakiwa hai ama miili yao kiasi cha kutia shaka kuwa huenda bado wamenasa ndani ya vyumba vya meli hiyo iliyozama chini ya kina kirefu cha mkondo wa bahari ya Hindi.
Tangu kuokolewa kwa abiria 619 na kuopolewa kwa miili ya watu 197 hadi jana jioni, hakujapatikana mtu hai ama mwili wa abiria aliyekufa maji ukielea juu ya maji ama kukokotwa kupelekwa mwambao mwa nchi kavu.
Katika eneo ilipo Meli hiyo zipo Meli nyingine za MV Kasa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na MV Mamba ya Jeshi la Polisi ambazo zote ziliwasili alfajiri siku iliyotokea tukio hilo la kuzam,a kwa MV Spice Islander.



Hata zoezi la kutafuta maiti za ndugu zetu wazanzibar halijaisha serikali inaruhusu kuwepo na sherehe na michezo kama kawaida kwa mfano michezo ya mpira umiss n.k
ReplyDeletetaifa limepoteza watu zaidi ya 200 inapaswa kushirikiana na waliofiwa na majeruhi katika hali au kipindi hichi kigumu cha maombolezo
nakumbuka alipokufa baba wa taifa kulikuwa na maombolezo ya mwezi mzima yani siku 30 bila muziki sherehe aina yeyote hata harusi zilikuwa zinafanyika kimya kimya
leo hii taifa limepoteza watu zaidi ya 200 lakini sherehe zinaendelea kama kawaida kwa kweli ni aibu kubwa kwa taifa
ankali weka hii watanzania waweze kujadili hii hali
Hivi kwa nini nchi yetu ina maziwa na bahari sehemu kubwa lakini
ReplyDeletetunakosa kuwa na wazamiaji angalau watano waliofundishwa vizuri
na wenye vifaa.
Jamani, nadhani sasa inabidi serikali ijiangalie upya na kuweka mkazo katika maandalizi ya kupambana na majanga yanayohusisha vyombo vya majini. Haiingii akilini nchi yetu bado inatekegemea waokozi/wazamiaji kutoka Afrika ya kusini. Tukio la MV Bukoba halijatufundisha kabisa.
ReplyDeleteNi kwa sababu gani basi nchi yetu haiwekezi kwenye uwezo wa kuokoa majini wakati ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na maji mengi barani Afrika???????. lake victoria, Nyasa, Tanganyika, Rufiji, Ruvuma na bahari ya hindi. Kote huku vyombo vya usafiri wa majini vinatumika na ambako ajali inaweza kutokea wakati wowote. Tatizo la kutokuwa na uwezo wa uokoaji wakati tumezungukwa na mazingira ya hatari ni kosa kubwa.
Jeshi letu (Navy) na Polisi ni wakati sasa wawekeze katika hili. wawekeze kwa kiwango cha kuaminika duniani/Afrika kiasi panapokuwa na majanga watu wetu wanaweza kuhitajika. Sababu ya kuanzisha na kuimarisha kitengo hiki tunazo, hii tuichukulie kama ni matayarisho mengine ya kivita au uvunjifu wa amani, kama tuliweza ku-iquip jeshi letu la polisi kabla ya uchaguzi, tunaweza pia kuanzisha na kuimarisha kitengo hiki. Lengo liwe ni kuokoa na siyo kuopoa maiti. Naamini kama kikosi hiki kingekuwepo maisha mengi yangeokolewa.
Tuamue.