Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu matumizi ya nembo ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na maonesho makubwa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanywa na Wizara hiyo eneo la Butiama, Musoma kuanzia tarehe 7-14 Oktoba na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki maonesho hayo na kuitumia nembo hiyo kwenye shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara .Kushoto ni Bw. Mulwa Msongo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu na Bw. Raphael Hokororo (kulia) Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari.
Msanii mkongwe wa Muziki nchini Tanzania kutoka Bendi ya Kilimanjaro (Njenje) Waziri Ally (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara litakalowajumuisha wasanii wakongwe (wazee) na wale wa kizazi kipya (Bongo Fleva) wapato 40 litakalofanyika katika ukumbi wa Diamondi Jubilee wakati wa kilele cha maadhimisho hayo tarehe 9 Desemba 2011 ambapo nyimbo mbalimbali zilizoimbwa kuanzia miaka ya 1961 – 2011 zitaimbwa kwa ushirikiano.
Msanii na kiongozi wa B. Band Banana Zolo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo) pichani kuweka msisitizo wa ushiriki wa wasanii wa kizazi kipya na wale wakongwe katika Tamasha la pamoja la maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Said Fella mwakilishi wa kundi la TMK Family (wa pili kutoka kushoto),Mzee King Kii (katikati) na Bw. Waziri Ally.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Sethi Kamuhanda ametangaza rasmi nembo ambayo itatumika katika madhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Bw. Kamuhanda ametangaza nembo hiyo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa wakati nchi yetu ikisherehekea miaka 50 ya Uhuru Serikali kupitia kamati ya kitaifa ya maadhimisho imeandaa nembo rasmi ya maadhimisho hayo.
Pamoja na ubunifu mwingine uliopo katika nembo hiyo, kuna ujumbe pia unaosomeka kuwa TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE.
Akieleza maana ya maneno hayo amesema kuwa kuthubutu ni kufanya jambo kwa ujasili na kusema kuwa, kwa ujasili mkubwa nchi Yetu imethubutu kudai uhuru, imethubutu kujenga umoja miongoni mwa wananchi, imethubutu kuwa na muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar na tumethubutu kujiletea maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Amesema kuwa katika masuala yote tuliyothubu tumeweza kuyafanikisha na ni dhahiri kuwa taifa limeendelea katika sekta mbalimbali na tunazidi kusonga mbele ili kujiletea maendeleo zaidi.
Aidha, amevitaka vyombo vya habari nchini kuhakikisha kuwa vinaitangaza nembo hii ili wananchi waweze kuielewa vizuri. Pia ameyataka makampuni ya watu binafsi kuhakikisha kuwa wanaitumia nembo hii katika maeneo yao na katika machapisho yao mbalimbali.
Wakati huhuo, amezungumzia suala la kufungwa kwa Uwanja wa Taifa baada ya mchezo wa Ngao ya Hisani uliochezwa kati ya Simba na Yanga tarehe 17 Agosti, 2001 kuwa baada mechi ile kulitokea uharibifu wa vifaa ambavyo vilihitaji matengenezo kabla ya matumizi ya Uwanja.
Bw. Kamuhanda ameeleza kuwa wataalam wa viwanja waliishauri Wizara kuwa uwanja ule unatakiwa kutumika si zaidi ya mara mbili kwa wiki kwa kuwa majani yale ni ya asili na yanahitaji kutunzwa.
Amesema kuwa Wizara imeshawasiliana na TFF kwa kuwa ndio wenye jukumu la kupokea maombi kutoka kwa vilabu kwa ajili ya kutumia uwanja ule, ili wanapoletewa maombi hayo wazingatie masharti ya matumizi ya Uwanja huo.
Ameeleza kuwa mechi za Kimataifa pamoja na zile zinazohusisha vilabu na Timu za kimataifa zitaruhusiwa kutumia uwanja huo lakini kwa kuzingatia ushauri uliotolewa na wataalamu wa viwanja kuhusu matumizi ya uwanja huo.



Huyo King Kiki jumamosi iliyopita me nimekwenda Laprima, nimelipa hela zangu kumbe mwenyewe hayupo kasafiri wako vijana wake tu wanatupigia mamndombolo tu. Nilichukia.
ReplyDeleteMzee Kiki tunapokuja Laprima tunakufuata wewe na zile za zamani Jakeline na Fransiska sio hayo mandombolo.
Tukiyataka hayo mandombolo kwani si tunakwenda tu Makumbusho?
Aaaa! Unatubowa bana!
Hii nembo wameipatapata vp? sisi wengine wajiriamali tulikuwa tunasubiri watangaze shindano la kubuni ili tushiriki ila naona kimya. Wananikumbusha nembo ya TCRA majuzi walivyotangaza full page kwenye magazeti shindano la milioni 5 wakaja kuzindua nembo siku ya submission.
ReplyDeletemsimsahau Steven Hiza alieimba TANZANIA YETU na Atomic jazz band
ReplyDeleteNuliza tanzania bara ilipata uhuru mwaka gani ? Mbona munatuchezea jamani ? Uhuru ni Wa Tanganyika sio tanzania,na kama munasherehekea uhuru basi tumueni bendera ya tanganyika sio tanzania ,bendera ya tanzania ni ya muungano tu,musitu foolish viongozi
ReplyDelete