Nyumba ya Waziri Chami ambayo watu wasiojulikana walibomoa na kufanikiwa kuiba vitu mbalimbali.
Eneo la mlango wa kuingilia katika nyumba ya Waziri wa viwanda na Ushirika Dk Cyril Chami linavyoonekana baada ya watu wasiofahamika kuvunja na kufanikiwa kuiba vitu mbalimbali.
Dada wa Waziri Chami ,Maria Chami akionesha mabaki ya vitu mbalimbali vya waziri Chami mara baada ya watu wasiojulikana kuiba nguo na vitu vingine vilivyokuwa chumbani kwa waziri huyo.
Na Dixon Busagaga,Moshi.
SIKU moja baada ya waziri wa viwanda na biashara Dk. Cyril Chami kumtaja kwenye mkutano wa hadhara mtuhumiwa namba moja wa tukio la kuvunja nyumba na kutishia maisha ya mama yake mzazi,mtuhumiwa huyo ameanza kutafuta mbinu za kutaka kuomba radhi kwa familia ya waziri.
Hatua hiyo inakuja baada ya watu wanaotajwa kuwa wasaidizi wa mtuhumiwa huyo aliyetajwa kwa jina la Valerian Ngowi maarufu kama Askofu, kutiwa nguvuni kufuatia msako mkali uliofanywa na kikosi kazi cha makamanda kutoka mikoa ya Mtwara na Dar es Salaam, wakishirikiana na askari polisi wa mjini Moshi.
Watuhumiwa hao wanne walikamatwa kwa nyakati tofauti usiku wa kuamkia jana Jumapili, ambapo mmoja kati yao alikamatwa akiwa amejificha uvunguni mwa kitanda chumbani kwake.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na mmoja wa wanafamilia ya waziri huyo zilisema kuwa Askofu amekuwa akipiga simu mara kwa mara kutaka kuiomba radhi familia hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa shilingi milioni tano, kwa ajili ya kugharamia uharibifu uliojitokeza kwenye nyumba hiyo.
“Askofu amekuwa akipiga simu mara kadhaa na alimtuma mtu kuja nyumbani kuomba kukutana na familia ili kuomba radhi na kulipa gharama za uharibifu uliofanywa kwenye nyumba ya kiongozi wetu”alisema mwanafamilia huyo.
Mwanafamilia huyo ambaye hakupenda kutajwa gazetini kutokana na vitisho ambavyo Askofu amekuwa akivitoa kwa wakazi wa kijiji cha Manushi alisema mtuhumiwa huyo amekiri kuishi kwa mashaka kutokana na kusakwa kila kona na askari polisi hali inayomlazimu kuomba msamaha.
Hata hivyo taarifa zilisema kuwa mtuhumiwa huyo anaogopa kufika kituo cha polisi kwa hofu ya kushikiliwa tena huku akieleza kuwa amekuwa mfungwa wa muda mrefu na asingependa kurudi huko.
Hata hivyo familia ya waziri Chami, imeelezea kusikitishwa na kitendo hicho, ambacho kimekuwa kero kubwa kwa wakazi wa kata ya Kibosho Magharibi, ambao wamedai kupata mateso makubwa kutoka kwa mtuhumiwa huyo anayetajwa kuwa tishio kwa raia.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Kibosho Magharibi wameunga mkono vita iliyotangazwa na waziri Chami dhidi ya mtuhumiwa huyo, na kusema kuwa kwa muda mrefu mshukiwa huyo amekuwa kero kwao, kwani amejihusisha na matukio kadhaa ya mauaji, unyanyasaji na udhalilishaji.
Taarifa zilisema kuwa mtuhumiwa huyo amewahi kuwajeruhi baadhi ya kinamama waliomtaja kuhusika kwenye matukio ya uhalifu, huku kukiwa na taarifa kwamba baadhi yao wamejeruhiwa na kuonywa kutotoa taarifa polisi au kwenda kutibiwa hospitalini.
Mbali na kujihusisha na vitendo hivyo mtuhumiwa huyo alidaiwa kuwapora wakulima mazao ya chakula wakati wa mavuno na kujilundikia nyumbani kwake.
Wachagaaa nomaaaaa mmmmmmh kazi iliyobaki
ReplyDeleteHongera waziri kwa kutangaza vita dhidi ya mhalifu ila vita hiyo ilitakiwa kutangazwa mapema sio kusubiri ujeruhiwe ndio upambane nae. Nina imani wananchi wake walitamani vita hiyo ianze mapema zaidi
ReplyDeleteMBONA HAO JAMAA WANAJULIKANAGA TANGU KITAMBO , NA WATAKAMATWA BUT TUKIENDA KUHESABIWA CHRISMASS TUTAKUWA NAO MTAANI NA WATATUIBIA TENA??????????
ReplyDeleteMANGI WA SINZA
kwani waziri hana walinzi wa jeshini au anakaa kambi ya fisi.
ReplyDeleteKwa kweli hali kama hii ni kawaida katika sehemu nyingi za Tanzania. Ukiwa nyumbani kwako unaweza kuvamiliwa na hata kupigwa, kufanyiwa vitendo vya kunyama na wahalifu.
ReplyDeleteBahati mbaya sana wahalifu hawa huwa wanawatishia raia wema na mara nyingi hutekeleza wanayosema kwa wale ambao hukiuka masharti.
Kuna kila sababu ya jeshi la polisi kuweka mazingira ambayo yatawalinda wanachi pale wanapoa taarifa za wahalifu.
Naingiwa na hofu kubwa, hikiona sasa wanafika hadi kuibia wakumbwa, hii maana yake wadogo wao walishalizwa sana.
Sifurahiii uhalifu ila wakati mwengine wakubwa wakiguswa basi kwa kiasi fulani amani hupatikan.
Mdau