Tume ya Uchaguzi iliyoendesha uchaguzi mdogo wa wabunge katika Jimbo la Igunga mkoani Tabora,imemtangaza Dkt. Dalali Kafumu (pichani) kuwa mshindi wa Ubunge wa Jimbo Igunga baada ya kuwashinda wagombea wenzake saba wa vyama vya Upinzani.


Matokeo hayo yametangazwa muda mfupi uliopita na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bw  Protase Magayane . Hivi sasa viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na wanachama wake wapo katika uwanja wa Sokoine kusherehekea ushindi huo.

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KIMEJIZOLEA JUMLA YA KURA  26,488 NA KUSHINDA KITI CHA UBUNGE KILICHOACHWA WAZI NA MH ROSTAM AZIZ ALIYEJIUZULU HIVI KARIBUNI.

CHAMA CHA  DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KIMESHIKA NAFASI YA PILI KWENYE KINYANG'ANYIRO HICHO KWA KUPATA JUMLA YA KURA 23, 260.

CHAMA CHA WANANCHI (CUF) KIMESHIKA NAFASI YA TATU KWA KUJIPATIA JUMLA YA KURA 2104.

KWA USHINDI HUO MGOMBEA UBUNGE WA CCM DR DALALY KAFUMU NDIYE MRITHI MTARAJIWA WA ROSTAM AZIZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE YAMEWASHUKA BWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA SASA WANA CCM KAZI MOJA KUKIIMALISHA CHAMA TUSIWAPE NAFASI WAPINZANI KUTUINGIZIA FITINA NA WANANCHI WAO KILA KUKICHA KAZI YAO NI HIYO SASA MWENDO MDUNDO KWA KUWATUMIKIA WANA IGUNGA YAANI MMETUKOSHA NASI TULIO UGHAIBUNI NA WAPENZI NA WAFUASI WA CCM mdau richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Kwa mtazamo wangu, CHADEMA wameshinda kichama kuliko CCM.

    ReplyDelete
  3. CHA DEMA WAMECHAKACHUA CHAKACHU CHAKACHU CHA. MIMI SIO MWANA CCM HATA KIDOGO. LAKINI KWA KITENDO CHA CHADEMA CHA KUMDHALILISHA NDUGU YANGU FATMA KIMARIO THIS IS WHAT THEY DESERVE. A HUMILIATION.

    ReplyDelete
  4. Nakuunga mkono ndugu yangu hapo juu Chadema kama chama cha siasa kimeshinda na CCM kama dola imeshinda pia kwani huwezi kuwa na mchezo
    ambao wewe kama CCM ukawa refarii, ukawa mchezaji na pia jaji.

    ReplyDelete
  5. chadema ilikuwa ikipambana na tasisi za dini,dola ,serikali,na vyama vya siasa.kwa mtizamo wangu from nothing to 23,000 ,cdm inaimarika!!!!! tusubirin 2015

    ReplyDelete
  6. chadema itakufa kabda ya 2015 wataishiwa mafuta kama cuf

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...