Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini
Mh. Godbless Lema
Na Woinde Shizza,Arusha

KESI ya kupinga matokeo ya ubunge wa Godbless Lema wa Jimbo la Arusha Mjini,imeahirishwa hadi Jumatatu ijayo baada ya mahakama hiyo kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu.

Akiahirisha kesi hiyo leo, Jaji Aloyce Mjulizi, alisema wakili wa walalamikiwa Method Kimomogoro,aliomba kupewa nakala ya uamuzi mdogo uliotupilia mbali pingamizi lililowekwa dhidi ya kesi hiyo.

Pia aliomba kupewa nakala ya mwenendo wa shauri hilo lakini hadi kesi hiyo inatajwa leo asubuhi upande wa walalamikiwa haukuwa umepata nakala hizo.

“Nathibitisha drafti na nakala ya mwenendo wa shauri la pingamizi ipo kwenye faili nilikabidhiwa leo,” alisema Jaji Mjulizi.

Katika uamuzi wake wa kuahirisha kesi, Jaji Mjulizi alimwagiza msajili wa mahakama kutoa nakala hizo kwa wadaiwa na wadai kabla ya kuanza kusilikiza kesi hiyo wiki ijayo.

Pia alimwagiza msajili wa wilaya kutoa taarifa ya shauri hilo kwa mujibu wa sheria na kubandika kwenye ubao wa matangazo mahakamani hapo na kuomba ukumbi mkubwa wa kusikilizia kesi hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu wanaopenda kwenda kusikiliza.

Maagizo mengine aliyotoa ni kumtaka msajili kuweka utaratibu wa mwenendo wa shauri hilo kusikilizwa kwa vipaza sauti ili kuruhusu watu wengine watakaoshindwa kuingia ndani ya ukumbi waweze kusikiliza.

Jaji Mjulizi alitoa amri hizo baada ya wakili wa wadai Alute Mughwai,kuikumbushia mahakama hiyo kuhusu muda uliopangwa kusikiliza kesi hiyo hadi Desemba kuwa ni mdogo.

Kutokana na hali hiyo aliomba mahakama hiyo iandae utaratibu wa kuomba muda wa nyongeza, kutoa taarifa ya siku ya kesi kwenye ubao wa matangazo, na kesi hiyo isikilizwe kwenye ukumbi mkubwa zaidi.

“Hiki chumba hakifai kwa usikilizaji wa kesi hii, tumejazana na hewa haitoshi, inatakiwa ipande toka chini hadi kichwani,” alisema na kuongeza,“tunahitaji uwanja mpana wa kufanya kazi yetu.”

Pia Wakili Mughwai alilalamikia suala la usalama mahakamani hapo lakini wakati akitoa ombi hilo, sauti za kumsonya zilisikika kutoka kwa watu waliokuwa wamekaa nyuma yake.

“Mheshimiwa Jaji, unasikia jinsi ninavyosonywa, hii inaonyesha wanataka nisiseme na huu sio utaratibu wa kuendesha kesi mahakamani,” alisema.

Hata hivyo, Jaji Mjulizi alisema, “hawakusonyi wewe ila wanaisonya mahakama,” na baada ya kusema hivyo watu hao walisikika wakipiga makofi,lakini baadaye Jaji alionya kwamba anayesonya anaidharau mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. habari qishinehi ,! siasa za bongo ,nazani huu ni u dictator wana , awana tofauti na ma terrorist ,tanzia akuna haki , akuna huuru.
    jamaa ndo hivyo tena kasha finish.
    mimi ndomana ni bora niwe mtumwa ulaya adi nitakapo kufa.
    mungu ibariki tanzania

    mdau paris

    ReplyDelete
  2. mdau hapo juu, nipo hapa france na simjui mtazania yoyote ebu nipe mawasiliano tuonane; kwa ajili ya mandeleo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...