Ankal Michuzi,
Nakuletea picha hizo ambazo, zinamwonyesha Dr. Kheri Goloka, Mwambata wa Afya katika Ubalozi wetu wa nchini India uliopo New Delhi, alipokwenda kumjulia hali, mtoto Sesilia Edward Okechi anaendelea na matibabu yake katika hospitali ya Escort Heart Institute iliyopo New Delhi, India. Kama unakumbuka vizuri mtoto huyu aliletwa nchini India kwa ajili ya matibabu kwa michango ya wasamalia wema, kupitia hospitali ya Regency, iliyopo Dar es Salaam wakishirikiana na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten. Aliyesimama kushoto kwa mgonjwa, mwenye koti jeupe ni Daktari wa mgonjwa, Dr. Ashutosh Marwal (Senior Consultant Cardiologist) wa hospitali ya Escort Heart Institute.
Hali ya mtoto Sesilia inaendelea vizuri na madaktari hospitalini hapo wanaendelea na uchunguzi wa tatizo lake la ugonjwa wa moyo ili wampatie tiba mwafaka.
Nawasilisha.
Mdau.
mwenyezi mungu atakulinda na sisi tunakuombea.
ReplyDeleteOh god is great, you will be fine soon god blees you
ReplyDeleteMwenyezi Mungu,mwenye uwezo kupita ufahamu wa mwanadamu,uliyemtoa mwanao wa pekee afe msalabani kwa ajili ya makosa yetu,na kwa kupigwa kwake Yesu pale msalabani,sisi tulipona.Namweka mikononi mwako mtoto huyu Sesilia,ukamponye sasa na ugongwa huu unaomsumbua,nawaweka mikononi mwako madakitari na wasaidizi wao wote wanaoshiriki kwenye zoezi zima la matibabu ya mtoto huyu.Wape ufahamu utokao juu ili mtoto huyu akapone kabisa.Nawaombea mbaraka wote waliotoa mali zao na msaada wowote katika kufanikisha matibabu haya, Mungu wazidishie neema na mafanikio katika shughuri zao za kila siku,naomba na kushukuru katika Jina la Yesu,AMINAAAAAAAA
ReplyDelete