Na Aboud Mahmoud

NGOMA ya Mpe Chungu kutoka katika kijiji cha Mzuri Makunduchi,ambayo kwa takriban miaka saba sasa imetoweka katika macho wa wanakijiji hao,imeonekana kuvuta mashabiki wengi katika mradi wa100% Zanzibari maarufu kwa jina la 'Shangiria Maridhiano'.

Katika mradi huo ambao limeandaliwa na Taasisi ya Swahili Perfomance Art Centre na kudhaminiwa na Ubalozi wa Norway na Kampuni ya simu ya Zantel lilifanyika katika uwanja wa Jamuhuri Makunduchi.

Ngoma hiyo ya Mpe chungu ilionekana kuvutia wengi hasa wananchi wa kijiji hicho kutokana na uchezaji wa ngoma hiyo huku wakitumia lahaja ya ambayo ndio inayozungumza kijiji hapo.

Mashabiki na wapenda burudani ya muziki wa kijiji cha Makunduchi walionekana kuvutiwa sana huku wengine wakishindwa kustahamili na kuanza kuserebuka uwanjani hapo.

Aidha kikundi cha taarab cha Maendeleo Music Taarab kuotaka Pemba, ambao ndiyo walikuwa wageni katika onesho hilo la Makunduchi, nacho kiliamshia hisia za hadhira waliofika katika eneo hilo hasa pale walipoanza kuimba nyimbo zao maarufu ikiwemo Zao la karafuu.

Pia nyimbo ya Lulu, Mgomba na Kitandawali zilizoneka kuvutia hadhira hiyo kutokana na umaarufu wa nyimbo hizo katika masikio na midomo ya wananchi wengi wanaopenda taarab.

Katika fani ya maigizo nayo haikuwa nyuma ambapo kambi ya wasanii hao kutoka kisiwani Pemba wakiongozwa na msanii maarufu, Khamis Nyange Makame 'Profesa Gogo' na wa kijiji cha Makunduchi ilifanikiwa kuteka nyoyo za mashabiki hao hasa pale wasanii hao walipoonyesha onesho lenye kuelezea kero zinazowakabili wananchi

Akizungumza na wananchi waliohudhuria katika muendelezo wa tamasha hilo,Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Mzee Haji Makungu Mgongo,amewataka wananchi wa kijiji hicho kuendelea kuyadumisha maridhiano hasa katika upande wa ngoma za utamaduni.

Amesema kuwa kuyaendeleza maridhiano yaliofikiwa na viongozi wa nchi ni kupata maendeleo mbali mbali ikiwemo kuitangaza sanaa na utamaduni wa nchi.

Mradi wa 100% Zanzibar 'Shangiria Maridhiano' wiki hii linatarajiwa kuhamia katika kijiji cha Kangagani kisiwani pemba ambapo wasanii mchanganyiko wa Taarab kutoka Pemba na Unguja watafanya kamb ya kisanii kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 25 hadi 29 Oktoba. Onesho la wiki hii litafanyika katika Uwanja wa skuli ya Kangagani siku ya Jumamosi tarehe 29 Oktoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...