Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma William Erio (katikati) akishikana mikono na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Mwinda Kiula-Mfugale wakati wa hafla ya chakula cha
jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau  waliokuwa wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa  PPF  jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni, Minnie Kibuta.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio (kulia) akishikana mikono na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi. Robi Matiko-Simba wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa wanachama na wadau  waliokuwa wakihudhuria Mkutano Mkuu wa 21 wa  PPF  jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja Mahusiano wa PPF, Bi. Lulu Melenge.
 Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni wa NBC, Bi. Minnie Kibuta akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na NBC kwa wadau wa PPF mjini Arusha mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wadau wa PPF wakifurahia vinywaji katika hafla hiyo pembeni ya jiko la moto lililowekwa kwa ajili ya hali ya hewa ya kibaridi iliyopo mjini Arusha kwa sasa.
 Kikundi cha wamasai kikitoa burudani katika hafla hiyo.
Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) Ofisa Uhusiano, Eddie Mhina na Mwenyekiti Mtendaji wa  Globu ya Jamii, Ankal,  wakibadilishana mawazo katika hafla hiyo mjini Arusha mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kiswahili shida, NBC yaandaa wakati inaonekana hapa hawapo kwenye maandalizi hii ni sherehe yenyewe

    ReplyDelete
  2. uncle mbona una nundu shavuni nini tena. Ahsante kwa updates you are the best!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...