Mke wa Rais wa Zanzibar
Mama Mwanamwema Shein
Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein amewataka kinamama wa Vikundi vya Ushirika kuzidisha maelewano katika vikundi vyao kwani ushirikiano wao ndio utakaoweza kujiletea maendeleo zaidi.

Hayo ameyasema leo huko katika Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini A wakati alipokuwa katika ziara ya kuhamasisha vikundi vya ushirika vya Mkoa huo.

Amesema kuwa amefurahishwa sana kupata nafasi ya kukutana na kinamama waliojikusanya pamoja katika kujitafutia maendeleo jambo ambalo ni muhimu kwani ndio njia pekee itakayowakomboa na kuwatoa katika umasikini.

Amewasisitiza akina mama hao kuwa kwa sasa sio wakati wa kubweteka hivyo ni lazima wafunge vibwebwe kwa kushirikiana na akina baba katika harakati za kukuza uchumi wa familia pamoja na nchi yetu kwa jumla.

Aidha amesema ni dhahiri kuwa utaratibu wa kujiunga pamoja kwenye vikundi, hurahisisha kupatikana kwa misaada kama vile mikopo na mafunzo mbali mbali.
Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Dk Shein imejiandaa kuwasaidia wananchi waliojiunga katika Vikundi vya Ushirika ambapo Wizara ya Kazi Uwezeshaji Kiuchumi na Ushirika kwa kushirikiana na Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana,Wanawake na Watoto zimetayarisha kutoa huduma hizo kwa lengo la kusaidia zaidi akinamama na kuwaomba wasiiache fursa hiyo.
Pia amewataka kinamama kusimamia malezi mazuri kwa watoto wao ili wapate vizazi vizuri na kuwaasa kutumia madawa ya kulevya ambayo yanaweza kuwapelekea katika maambukizi ya Ukimwi na mimba za utotoni.

Halikadhalika Mama Mwanamwema Shein ametoa Msaada wa Vitu mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili Laki Tatu Sitini na Moja Elfu kwa Vikundi 25 vya Jimbo la Nungwi ikiwemo charahani ,khanga mipira ya maji ,mbolea ,ukindu na kamba za kupandia mwani.

Katika vikundi hivyo ni pamoja na ni nungwi saccos,kigunda saccosfukuchani saccos , wavumilivuna mungu tupe kheri.

Wakati huo huo Mama Mwanamwema Shein aliendelea na ziara yake katika Jimbo la Mpendae na kukagua vikundi vya ushirika vya Jimbo hilo na kujionea mambo mbali mbali ikiwemo mikoba mikeka na aina za mbogamboga kama vile Mronge na Mtoriro zinazolimwa na vikundi hivyo.

Vikundi hivyo vya Jimbo la Mpendae vilizawadiwa jumla ya Shillingi Millioni Mbili na lakinne kwa vikundi kumi na sita vya jimbo hilo.

Kwa upande wa Wanavikundi hao wamemshukuru Mama Mwamamwema shein kwa kuwatembelea na kuwazaadia zawadi hizo ambazo zitawasaidia katika vikundi vyao.

Katika ziara hiyo Mama Mwanamwema amefuatana na Mama Asha Balozi Mke wa Makamo wa Pili wa Rais, Mama Fatma Karume na Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Unguja,Wakuu wa Wilaya na wake wa waheshimiwa Wabunge na wawakilishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...