Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imeziruhusu rasmi Meli za MV SERENGETI na M.V SEPIDEH kusafiri baada ya kuridhika na Ukaguzi walioufanya hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Haji Vuai Ussi, amesema hayo leo huko Afisini kwake wakati alipokuwa akitoa taarifa juu ya kukamilisha taratibu zote zilotakiwa na Mamlaka hiyo waliopangiwa ili Meli hizo ziruhusiwe kuanza kufanya safari hizo baada ya kuzuiliwa.

Amesema kuwa kuanzia hapo kesho Meli hizo zitaendelea na Safari zake za kawaida kwa Meli ya M.V Serengeti kufanya safari za Unguja na Mkoani Pemba na SEPIDEH itafanya Safari zake Dar es Salaam, Unguja na Pemba.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa awali vyombo hivyo vilizuiwa kufanya Safari zake kutokana na Hitilafu za kiufundi katika mashine, jambo ambalo lilikuwa likitishia usalama wa Abiria na mali zao.

Ussi amewaomba Wananchi kuondowa hofu ya kuvitumia vyombo hivyo kwani kwa sasa viko salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. baada ya baala kubwa kutokea sasa ndio wanafanya ukaguzi wa boats, kwangu it doesn't make sense at all! ila tuangalie hawa jamaa wana akili kama wadudu kesho kutwa watasau na balaa litaanza vile vile(boat baada ya kupakia watu 500 wataendelea kupakia watu 3000) nahisi hawa wamiliki wa boat zinazoanza safari Dar serikali lazima iwalazimishe wawe na software maalum kwa ajili ya biashara zao(kwenye kuuza ticket zao) bila ya hivyo hali itaenedelea kuwa vile vile...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...