Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akiwa Ofisini kwake tiyari kwa kuanza kazi mara baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe. Daniel Ole Njoolay. Miongoni mwa mambo aliyoahidi kuyafanyia kazi kwa ukaribu ni kutatua kero za wananchi pamoja kuwawajibisha viongozi wenye utendaji mbovu wanaochelewesha maendeleo ya Rukwa.

Mhe. Injinia Stella Manyanya akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Rukwa Mhe. Daniel Ole Njoolay. Aliwaasa wanarukwa kujiamini na kuunganisha nguvu zao ili waweze kuwekeza katika rasilimali nyingi zinazopatikana mkoani hapo zikiwepo utalii, uvuvi, kilimo, madini, ufugaji na biashara.

Mhe. Injinia Stella Manyanya akisaini nyaraka muhimu za makabidhiano wakati alipokabidhiwa rasmi majukumu ya kuuongoza mkoa wa Rukwa, anayeshuhudia ni aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe. Daniel Ole Njoolay.
 Picha na Hamza Temba, Afisa Habari Rukwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hivi huu mtindo wa mtu mmoja kuwa nyazifha zaidi ya moja utaisha lini hapa TZ. Mbona tuna wasomi wengi tu??

    ReplyDelete
  2. Nyazifa nyengine hulipwi mshahara. Hakuna mshahara wa mwenyekiti wa bodi!!

    ReplyDelete
  3. Ankal kiswahili cha engineer ni mhandisi.

    ReplyDelete
  4. Tz kero tupu hakuna tunalolijua katika administrating approach.Yaan mkuu wa mkoa hawezi kuwa mbunge mzuri coz atakuwa anachanganya uchama wake wa ccm wakati watu anaowaongoza ni wa vyama vyote pamoja na wale wasikuwa na vyama.Tubadilikeni jamani.Ewe Katiba mpya tuokoe sisi waja wako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...