Na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar 20/10/2011

WAKATI kindumbwe ndumbwe cha ligi darala la kwanza Taifa kikiendelea tena leo, timu ya malindi  ya Zanzibar  imeendelea na  azma yake ya kususia ligi daraja la kwanza taifa baada yakutoonekana katika viwanja  vya Ngome vya Fuoni mjini hapa kwa ajili ya mchezo wa ligi  hiyo kati ya Malindi na  sharp boys

Kutokufika kwa timu hiyo kongwe  ya Malindi  kucheza ligi hiyo ya daraja la kwanza katika kiwanja cha Ngome cha Fuoni nje kidogo ya mji wa  Zanzibar kunatokana na madai kadhaa ambayo timu hiyo iliyowika miaka ya nyuma kabla haijateremka daraja  

Timu hiyo nguli ya Malindi ya Zanzibar inadai kwamba ligi ndogo ya soka ya Zanzibar haikukamilika kwani imechezwa kwa mkondo mmoja jambo ambalo ni kinyume.

Kufuatia kitendo cha timu ya Malindi kutokufika katika   kiwanja cha  Ngome washabiki wa mpira wameelezea masikitiko yao kuwa kitendo hicho kilichofanywa na timu hiyo kubwa cha kuendelea  kukacha kufika kiwanjani hapo si kitendo cha kiungwana.

 Katika sakata hilo la kutokushuka dimbani kwa timu hiyo ya Malindi shabiki mmoja alisikika akisema kuwa timu ya malindi ipo sawa sawa kwani ni kweli ligi iliyotakiwa kuchezwa mikondo miwili imechezwa mkondo mmoja jambo ambalo ni kunyume.

 Mashabiki wa mpira wa miguu walifikiria kwamba mgomo kwa timu ya Malindi umekwisha lakini hawakuamini macho yao kwa timu hiyo kutofika kiwanjani hapo kwa ajili ya kucheza ligi hiyo ambayo ngarambe zake zimeanza jana katika viwanja mbali mbali.

Mabingwa hao wa soka wa zamani wa Tanzania na Zanzibar katika mechi ya jana walikuwa wapambane na timu ya sharpboys ya Nungwi lakini kwa mshangao wa wengi timu hiyo haikutokea kwa ajili ya mechi hiyo ya ligi daraja la kwanza taifa

 Hata hivyo hayo yakiendelea ya sakata la Malindi kutokushuka kiwanjani timu ya Mtende Rangers ilifanikiwa kuifunga timu ya Kijichi Stars kwa 1-0 katika kinja cha Dimani

Bao hilo pekee lilowapatia  alama tatu  timu ya Kijichi stars lilifungwa na Ubwa Abdul  Omar na hivyo kuifanya timu hiyo kufikisha alama tisa.

Ligi hiyo inaendelea tena leo kati ya timu  ya Black Sailor watakao kipiga na timu  ya kikosil cha  jeshi la valantia KVZ wakati timu ya Ngome ya Fuoni itapepetana na timu ya JKU  katika kiwanja cha Ngome chaFuoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...