Kwa mara ya kwanza katika hitoria ya Tanzania,waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania wakiongozwa na mwalimu wa muziki wa injili afrika mashariki bwana John Shabani, chini ya usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita) wamekamilisha video ya wimbo ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.

 Pamoja na waimbaji mbalimbali kushiriki katika wimbo huo pia yumo bwana Masanja mkandamizaji, Stara thomas pamoja na mheshimiwa Martha Mlata ambaye amechangia sana katika kufanikisha kurekodi ya wimbo huo. 

Baadhi ya mambo aliyoyafanya Mh. Mlata ni pamoja na kufanikisha kupata sare na bendera kutoka serekalini pamoja na kutoa feha za kufanikisha kurekodi video hiyo. 

Pia studio ya Pro arts ya jijini Dar es salaam ilijitolea kurekodi sauti. Wazo la kuwakusanya waimbaji wa injili na kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru, lilianzishwa na bwana Tc Timothy Chelula na kumshirikisha mwalimu John Shabani, ndipo walipo kihusisha chama cha muziki wa injili na vyombo mbalimbali vya habari.

 Wimbo huo umepongezwa na wengi, kwani ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania na pia kitendo cha kuwakusanya waimbaji pamoja kimewabariki wengi. 

Muda si mrefu wimbo huo utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Baadhi ya waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:
1. Gloria kilahiro 18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro 19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji 20 Jane Misso
4. Upendo kilahiro 21 Addo November
5. Stella Joel 22. Martha Mlata
6. Nely Nyamanga 23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni
8. Bony Mwaitege 24. Douglas Pius
9. John Shabani 25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza 26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud 27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki 28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe 29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi 30. Joseph kasigala
15. Christina Matai 31. Debora Said
16. Tina Marego 32. Stara Thomas
17. Martha Mwaipaja 33. Victor Ahron
Na wengine wengi.
Pia waimbaji wa nyimbo za injili nchini wameshauriwa kujiunga na chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita), Kuna faida nyingi sana za kujiunga na chama. 

Fomu sasa zinapatikana kwa viongozi wa chama hicho. Kwa mawasiliano zaidi 0754 818767, 0716560094 au watembele www.johnshabani.blogspot.com
Mh. Martha Mlata akiwa katika picha ya pamoja na Masanja Mkandamizaji na waimbaji wengine wa muziki wa injili wakati wa kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
Waimbaji wa muziki wa injili nchini wakiimba kwa pamoja wimbo huo wakati wa kuurekodi.
Masanja Mkandamizaji akiimba wimbo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nimefurahi kusikia Mzee Makasi yuko hai na bado anaimba. Huyu tangu tuko Primary alikuwa ni mwanamuziki.

    ReplyDelete
  2. jamani wadau kuna kwaya dodoma ilikua inaitwa uvuke, naomba muitafute. ukiwasikia ata kama wewe nimpagani siku iyo utamkubari yesu. miaka ya tisini walikua wanatetemesha ardhi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...